Raila Odinga anasema Wakenya hawataketi nyuma huku Rais William Ruto akidaiwa kusimamia vibaya nchi. Alitoa mfano kutoka kwa utawala wa rais wa zamani marehemu Daniel Moi, ambaye enzi yake ilidumu kwa zaidi ya miongo miwili, ambayo alisema ilishindwa.
Waziri mkuu huyo wa zamani, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM, alisikitika kwamba rais alikuwa akipenya ndani ya Bunge la Kitaifa na kuathiri mchakato wa kutunga sheria huko.
Akiongea mjini Bungoma Raila alisema Marehemu Daniel Moi alikua na mamlaka mengi kwa kuwadhuru raia wake lakini hatimaye alitiishwa.
Alisema wakenya hawatasalia nyuma kwani Ruto alichukua njia hiyo.