Deni la serikali ya Tanzania linaendelea kuongezeka kila mwezi kwa kiasi cha dola milioni 544.8.
Haya yamo katika ripoti ya iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo imeeleza pia kuwa, kufikia mwezi Oktoba mwaka huu, Tanzania ilikuwa inadaiwa shilingi trilioni 64 ikiwa ni deni ambalo nchi hiyo inadaiwa na nchi au wafadhili wa nje, kiwango ambacho ni sawa na asilimia 70.6 ya deni la jumla la serikali. Wakopeshaji wa ndani wanadai serikali shilingi trilioni 26.6.
Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo, sekta ya uchukuzi na mawasiliano inaongoza kwa kiasi kikubwa cha deni, ikifatiwa na huduma kwa jamii, elimu, nshati na madini. Wakopeshaji wakuu wa ndani ya nchi ni kutoka kwa mfuko wa pensheni pamoja na benki za biashara, ikiwa inafikia kiwango cha asilimia 55.8 cha deni la jumla la serikali.
Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, alisema mwezi Juni mwaka huu kwamba, ongezeko la deni la serikali linatokana na kuongezeka kwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Serikali ya Tanzania imesema kwamba japo deni la linaendelea kuongezeka, ina uwezo wa kulipa.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, gharama za maisha kkatika nchi hiyo ya Afrika Mashariki zimepanda kwa kasii katika miezi ya hivi karibuni.
Wananchi wa Tanzania hivi sasa wanalalamikia kupanda kwa bei za vyakula huku kukiwekko na wasiwasi wa kutokea njaa katika baadhi ya maeneo hasa kutokana na mvua kuchelewa kunyesha.