Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijuma – 22nd March, 2024
Hotuba ya 1: Dua ya Imām Sajjad (‘a) -Ramadhan ni kipimo cha kutenganisha baina ya waumini na wanafiki
Hotuba ya 2: Saumu huipa nguvu nia ili kuweza kusimamisha udhalimu
Kwa ajili ya kupata Taqwa fursa ambayo Allah ameitoa moja ya fursa ya upendeleo zaidi ni mwezi wa Ramadhan. Ndani ya mwezi huu ameainisha wajibu fulani na kuamuru kutenda baadhi ya matendo.
Imam Sajjad( ‘a) anaendelea katika dua hii
وَالْحَمْدُ لِلّه الَّذِي جَعَلَ مِنْ تِلْكَ السُّبُلِ شَهْرَهُ شَهْرَ رَمَضَانَ،
Na kila sifa njema anazistahiki Allah ambaye amechagua kutoka miongoni mwa njia hizo mwezi wake, Mwezi wa Ramadhani
شَهْرَ الصِّيَامِ، وَشَهْرَ الإِسْلاَم، وَشَهْرَ الطَّهُورِ،
sifa yake ya kwanza ni mwezi wa kufunga, sifa yake ya pili ni mwezi wa Kiislamu na ni mwezi wa kujisafisha
وَشَهْرَ التَّمْحِيْصِ، وَشَهْرَ الْقِيَامِ،
ni mwezi wa kuwa kwenye majaribu, ni mwezi wa kusimama kwa ajili ya ibada
الَّذِي أُنْزِلَ فِيْهِ الْقُرْآنُ هُدىً لِلنَّاسِ،
“ ambao ndani yake imeteremshwa Qur’an ambayo ni muongozo kwa watu
وَبَيِّنَات مِنَ الْهُدى وَالْفُرْقَانِ،
Na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi
Imam Sajjad ( ‘a) anaelezea mwezi mtukufu wa Ramadhani kama njia ya kufikia radhi ya Allah.
Sifa ya kwanza ya mwezi huu ni kwamba ni mwezi wa saumu ambayo0 ni kitendo na ni ibada. Tafsiri ya Saumu sio kufunga. Inabidi tujaribu kutumia kama ilivyo katika istilahi ya Qur’an kama tunavyo tumia kwenye Zakāt, Hajj. Hivi ndivyo tunavyo takiwa kutumia neno saumu na salat. Tutazungumzia athari na malengo ya saumu katika hotuba ya pili. Moja ya funguo muhimu zaidi za kuweza kuifanyia kazi Taqwa ni saumu. Imam (‘a) naelezea ya kwamba huu mwezi ni mwezi wa Uislamu. Moja ya maana za Uislamu ni dini na maana ya pili ni ya kiistilahi ambapo inamaanisha kujisalimisha moja kwa moja, maana yake ni kukubali kila kitu ambacho Allah kakiamrisha bila ya masharti na pasina kuhoji swali lolote. Kwa wale ambao huleta visingizio wakati wa kutekeleza majukumu hiyo inakuwa ni dalili ya kutojisalimisha . wanaonyesha kwa njia nzuri kwamba sisi hatukubali maneno yako. Baadhi ya watu husema kwa uwazi kwamba hatutafanya hiki ambapo ni Kufr -e-Sari ( kukataa kulikokuwa wazi), na kukataa kwa pili ni kukataa kwa njia ya kuleta visingizio katika hali ya kiuungwana. Huku kote ni kukataa. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kujisalimisha. Ni mwezi wa Uislamu na ni mwezi wa kwenye kutii maamrisho ya Allah kabisa. Imekuja katika baadhi ya hadithi na kama zilivyo tafsiriwa kwamba mtu anatakiwa kujisalimisha kwa Allah kama mwili wa maiti unavyo jisalimisha kwa waoshaji josho la maiti. Tunatakiwa kuelekea popote pale ambapo Allah anaelekeza nyuso zetu, na tunatakiwa kuacha kuelekea asipopapenda Allah. Kinyume cha utiifu na kujisalisha ni uasi na huu ni mwezi wa kujitakasa. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kujitakasa. Kama vile tunavyo safisha nguo zetu na kuziweka safi pia. Kuna tofauti kati ya kujitakasa moyo na usafi wa nje. Usafi wa nje unamaana ya kuondoa uchafu mwilini. Na kujitakasa inamaanisha kuondoa uchafu wote ambao haukubaliki katika asili ya mwanadamu. Wudhu, ghusl na Tayammum hivi vyote hutakasa. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kujitakasa kwa ajili ya kutakasa nafsi kutokana na uchafu wa kiroho. Allah ametoa wenzo huu ndani ya mwezi wa Ramadhani ambapo nafsi ya mwanadamu hutakatishwa kiukamilifu. Hajj na Ramadhan ni matukio mawili ambayo ndani yake nafsi ya mwanadamu husafika. Huwa tunasafisha nguo zetu na miili yetu kimazoea. Sehemu hizo maalumu za mwili huchafuka na kuna jambo la tatu ambalo ni uwepo wako. Mwili na nguo hivyo viwili vyote ni vazi la nafsi. Je nafsi haitakiwi kusafishwa? Kama inavyokuwa mwili umechafuka na mafuta na kuvaa nguo safi bila kujisafisha mwili, hivyo basi nguo hizi safi hazitausafisha mwili bali nguo zenyewe zitachafuka pia.
Kisha Imam (a?) anasema mwezi huu umewekwa kwa ajili ya Tamhis ( تمحيص) neno hili hutumika pindi mambo yanapokuwa yamechanganyika. Ni kama ngano inapokuwa imechanganyika na uchafu na kokoto. Kuondoa uchafu kutoka katika kitu halisi ni Tamhis. Ni sawa na mwanadamu anapochafuka kwa uzinifu hasa ndani ya jamii ambapo watu wa aina tofauti huishi pamoja. Kutenganisha vitu ambavyo vimechanganywa pamoja ambavyo hupunguza thamani ni Tamhis. Ndani ya mwezi huu uchafu ambao unakuwa ndani ya mtu mwenyewe hutenganishwa na wa jamii. Katika mwezi wa Ramadhani tunaweza kumpata aliyekuwa muumini na mnafiki. Ikiwa mtu ataitekeleza Ramadhani kwa ukamilifu wake, kama kutimiza masharti ya Saumu. Na yule ambaye huleta visingizio vya uongo kutoka kwa madaktari ili asifunge sio muumini na hili hutambulika kutokana na mwezi wa Ramadhani. Ndani ya mwezi wa Ramadhani huja kipambanuzi cha kumjua ni nani muumini. Uchafu ambao huchukuwa nafasi ndani ya nyoyo zetu husafishwa. Tunapata nia chafu. Wakati tunapotenda kwa nia safi siku inayofuata nia hiyo huvunjika.
Shetani ni kiumbe ambaye anafanya kazi kwa watu wote kwa wakati mmoja. Huyu ni Shetani ambaye yupo sehemu zote kama tunavyo mtafsiri. Hii ina maana kwamba Shetani ana nguvu kubwa kama anavyoweza kuwafikia wengi kwa hali ya juu, utambuzi wake juu ya nia. Anajua kila anacho fikiria kila mmoja. Shetani mmoja tunayemzungumzia ni Ibilisi ambaye ana nguvu sana. Chanzo cha nguvu cha pili ni dhati ya Allah. Katika viumbe kuna baadhi wamenyimwa ( wana mapungufu), baadhi wana nyenzo na wengine hawana. Na mahusiano yao na Allah ni tofauti. Wafuasi wa Shetani wameweka msingi kwamba hakuna ugumu katika kuwa karibu na Shetani. Kuwa karibu na Allah ni ngumu na Shetani hajaweka masharti yeyote. Kadiri unavyofanya maovu mengi waovu na Shetani na watakupa nguvu. Sisi pia hukubali bila kukusudia ya kwamba Shetani ni nguvu ambayo mwanadamu hawezi kuitawala na mwanadamu hawezi kumshinda Shetani. Qur’an pia imemtambulisha Shetani na kuelezea maana yake pia. Shetani sio jina la Ibilisi ambaye ni jini bali ni sifa. Kama Dereva, na Rubani sio majina ya mtu bali ni uwezo ambayo unaweza kukua ndani ya mtu yeyote. Huu ni ujuzi, uwezo na sifa. Ushetani pia ni sifa ambayo inaweza kuwa kwa yeyote na kuchukua sifa hii. Shetani ni yule aliyetengwa mbali na anafanya kazi ya kuwaweka wengine mbali na Allah.
Tumewekwa mbali na njia ya Allah mara nyingi. Inabidi ufikiri ni nani alikuweka mbali na Allah? Hakutakuwa na jina la jini yeyote, inawezekana akawa mtu ambaye yupo karibu na mtu. Shetani yupo miongoni mwa marafiki zako na watu wako wa karibu ambao hukuweka mbali na Allah. Wale ambao ni wageni kwetu hawawezi kutuweka mbali na yeyote. Wazazi hutuchukua kutoka kwa Allah lakini wakati huo huo wanatuweka mbali na Allah. Wazazi wengi wamewafanya watoto wao kuwa mafisadi, kupata elimu a upotofu kwa kutoa ada kubwa. Shetani wa kwanza wa kumtenga mtoto mbali na Allah ni wazazi. Kuna wanafunzi wengi hapa ambao wamenunuliwa na watu, lakini kuna wengine ambao wamewaweka mbali na Jamea. Hawa ni mashetani ambao huwasilisha vitu ndani ya Jamea ili kuwachukua wanafunzi mbali na jamea. Kama unavyoweza kuwa unasoma kitabu kizuri halafu akaja mtu na kusema unapoteza muda wako kwa ajili ya kitu gani? Ulikuwa unafanya kitu kizuri na baadhi ya marafiki wakasema unafanya nini. Ulikuwa unaenda kusali sala ya jamaa na baadhi ya marafiki wakasema unaweza kusali mwenyewe nyumbani. Hawa ndio mashetani wa kweli wanao tuzunguka. Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani tunapata uhuru kutokana na Shetani huyu kupitia Tamhis. Katika mwezi wa Ramadhani Allah huwatenga waumini na Shetani. Mfumo na mkakati ambao Allah ameuweka katika mwezi huu humtenga Shetani. Leo waumini na Mashetani wanaishi pamoja. Hivyo amali za Ramadhani zimewekwa ili tuweze kumjua Shetani.
Kisha mwezi huu ni mwezi wa Qiyam ambayo ni istilahi ya msingi ya Qur’an. Katika kanuni hizi za msingi mojawapo ni Qiyam, inabidi tuchambue aya zote ndani ya Qur’an ambazo ndani yake neno hili limetumika. Qiyam ni kwa ajili ya Allah ambapo anasema ninakunasihini kwa jambo mmoja tu, ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wawili-wawili na mmoja -mmoja. Sawa sawa apatikane mtu wa kukuungeni mkono au asipatikane mnapaswa kusimama katika njia ya Allah. Haya ni mahubiri tu na nasaha kutoaka kwa Allah. Qiyam nyingine ni kuamka kijamii. Katika maendeleo ya mtu binafsi au maendeleo ya jamii, ili kufanya mapinduzi ya kusiamaisha mfumo wa Mwenyezi Mungu katika jamii unahitaji kufanya Qiyam. Nimewahi kutaja hapa kuhusu Ayatullah Yahya Noori ambaye alikuja Pakistan wakati wa mapinduzi. Mmoja katika wakuu wa Ahli Sunna alimuuliza mliwezaje kuleta mapinduzi. Alijibu kwa uzuri sana kwa lugha ya Kiarabu kwamba tulifanya mambo matatu, Qumna ( Tulisimama), Aqamna ( tuliwafanya wengine waamke) wastaqamna ( na tulibaki na msimamo). Iqama ya sala, Imamat hivi vyote vinahusiana na Qiyam. Iqamatu Sala inabidi kufanyika ili kuisimamisha dini. Kusimama kwa ajili ya Allah, mwezi wa Ramadhani ndio warsha kwa ajili ya haya. Katika mwezi huu hujifunza Qiyam. Baadhi ya watu husema kwamba Slalatul Layl ni Qiyam, hii ni rejea ya kimalengo. Qiyam ina maana ya kusimama katika njia ya Allah.
Huu ni mwezi wa kushushwa Qur’an. Kushuka kwa Qur’an tumekuelezea mara nyingi lakini kunahitaji kurudia. Nuzul ina maana ya kitu kinachokuja chini kutoka sehemu ya juu. Kushuka Qur’an maana yake ni Elimu itokayo kwa Allah. Kuileta katika kiwango cha ufahamu wa mwanadamu na ufahamu ndio Nuzul. Jambo hili hushika kasi na kufanyiwa kazi katika mwezi wa Ramadhan. Katika mwezi huu mbegu ya uongofu hupandwa katika moyo wa mwanadamu. Tunasoma Qur’an kwa ajili ya kupata thawabu ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuwa kivutio na sio lengo ambalo ni uongofu. Wenzo wa kuvutia humleta mtu karibu na Qur’an na kisha Qur’an humdhibiti mtu. Allah aliishusha Qur’an kwenye moyo wa Mtume (s.a.w) na kutoka kwenye moyo wa Mtume( s.a.w) ambapo inatakiwa kushuka katika nyoyo za waumini. Qur’an imesema na Ima (a) kwamba ni muongozo kwa wanadamu, lakini ukifanya utafiti kwenye umma unaweza kuona ni watu wangapi ambao wanakubali kwamba Qur’an ni kitabu cha uongofu?
Wakati huu sauti ya Qur’an ndio ipo juu ya nyimbo zote. Baada ya hili ni Naat kisha kufuatiwa na zile nyingine za kiulimwengu. Hakuna ambaye anaweza kuzalisha hizo zaidi ya Qari ( msomaji) wa Qur’an. Hili aliambiwa Mtume(s.a.w) kwamba maneno, na sauti zitabaki lakini muongozo hautabaki. Kama tunapata muongozo kutoka kwenye Qur’an basi inabidi mtosheke kwamba unapata kile ambacho Qur’an inakusudiwa. Ikiwa kinyume chake basi maana yake unaitumia Qur’an kinyume na mwelekeo ambao imekuja nao Qur’an. Sifa nyingine ya Qur’an ni kwamba imetoa mwanga ushahidi ulio wazi na uongofu. Ikiwa mtu atafanya juhudi ya kuifahamu Qur’an hatapata shaka ndani ya Qur’an. Kuna ushahidi ulio wazi wa muongozo wa Qur’an. Sifa ya Qur’an ni kwamba ni Furqan, ambayo hutenganisha baina ya haki na batili. Qur’an ni kipimo ambacho kwacho mtu anaweza kupambanua baina ya haki na batili. Inabidi kutathmini kila kitu kama vile akili, jamii, hadithi na Sunna kwa kipimo cha Qur’an na hapo utafahamu elimu ni nini, ujinga ni nini, ukweli na uongo. Kipimo hiki cha ukweli na uongo Allah amekitoa katika mwezi wa Ramadhan. Hiki ni kipindi cha kupandikiza mbegu ya Qur’an ndani ya mwezi huu.
Hotuba ya 2
Sawm (kufunga) ni mpangilio mmoja wa Ramadhani
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ {183}
Enyi mlio amini mmeandikiwa Sawmu kama walivyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha Mungu
Taqwa inahusiana sana na Sawmu. Taqwa ambayo ni mfumo wa ulinzi ambao mtu inabidi autengeneze mwenyewe na kwa ajili hii mwanadamu anahitaji nguvu moja. Nguvu hii humjia mwanadamu kutoka kwenye Sawm. Nguvu ya mtu sio kwa mwili wake bali ni kwa utashi ( irada). Na nguvu ya mwili pia hutokana na nguvu ya utashi. Tunaweza kuona watu wenye miili mikubwa yenye nguvu lakini hawawezi kufanya kitu chochote na hivyo kinyume chake kuna watu ambao wana miili dhaifu lakini wanafanya mambo makubwa na magumu ya kushangaza kutoka na nguvu ya utashi wao. Na siri ya nguvu za Allah ni utashi pia ambayo Allah hakumpa kiumbe mwingine yeyote zaidi ya mwanadamu. Kama tutatizama ulimwengu unao tuzunguka tutawapata watu waliofaulu na waliofeli katika kila nyanja. Kati ya watu milioni 250 , tunaweza kuona ni watu wangapi wamefanikiwa katika uwanja wa kielimu na kufikia daraja za juu za elimu na hadhi. Hakuna shida lakini ukitaka kutafuta utapata hasira. Ni wachache sana, na je siri ya mafanikio ni ipi? Kama Qarun wakati huo alikuwa kama Bill Gates na Ambani. Walifanikiwa vipi? Kuna mtazamo wa Qarun alisema kwamba nimepata kutokana na elimu yangu, hekima na akili. Kama utachanganua kwa uwazi zaidi utagundua kuwa njia aliyoiweka Allah katika mafanikio ya kimaada kidunia ni katika uthabiti wa nguvu ya utashi. Kila mtu ana shuku ya kufanikiwa kimaada lakini hawafanikiwi kwa sababu hakuna nguvu ya utashi ndani yao. Watu wachache ambao wana mafanikio ni wale ambao wamerithi kutoka kwa wazazi wao. Wengi wao ni wanaofanya juhudi na siri ya mafanikio ni nguvu ya utashi. Hivyo basi, mafanikio hata kama ikiwa ni kwenye mambo ya kimaada, kijamii au kiroho siri ya mafanikio inabaki kuwa ni moja nayo ni nguvu ya utashi. Nguvu ya utashi wetu ( irada) ni dhaifu. Ikiwa nguvu ya utashi itakufa kwenye watu milioni 250 watakuwa wapo zero watupu na mkabala wake ikiwa nguvu ya utashi watakuwa nayo watu 25 je wanaweza kufanya maajabu?
Jambo muhimu sana la kutia nguvu utashi ni Saumu. Namna gani Saumu itaimarisha nguvu ya utashi? Maana ya Kiarabu ya Saumu ni Imsak. Yote mawili yana maana ya kuacha, weka tofali wakati ukiendelea kufanya kazi nyingine. Kuzuia viungo vyenu , ndimi, mikono , maneno na vyakula ndio Saumu. Ulikuwa ukila mchana kutwa na sasa unatakiwa kuacha. Hivyo ni vipi kuacha kitu kunaongeza nguvu ya utashi? Mwanadamu ni mgumu wa kufanya jambo lakini pia ni vigumu sana kwa mwanadamu kuacha kufanya jambo fulani. Inahitajika nguvu ndogo kutazama lakini kufumba macho kunahitaji nguvu zaidi. Kuinamisha macho chini wakati anapo pita na maharam, na kuacha kuchunga ni ngumu zaidi. Hawawezi kudhibiti mambo ambayo yanakuja kutokana na ulimi. Kuacha mambo halali huimarisha nguvu ya utashi. Kuna watu ambao hushika njia wanapokutana na magumu, hubadilisha nia zao na nguvu ya utashi. Nguvu ya utashi huimarishwa na Saumu. Unapoikuza nguvu ya utashi kwa kuacha , kisha unaweza kuwafanya wengine waache pia.
Ndani ya mwaka huu watu wanafunga, wanaandaa na kutoa huduma ya futari, wanatoa sadaka, wanafanya dhikiri, wanasali , Tarawehe, wanasoma Qur’an na wanahudhuria katika sala za jamaa. Ukiwauliza watu wote hawa kuwa je mnaweza kumzuia Israel na Amerika kwa dhuluma ambayo wanafanyiwa Waislamu. Hawawezi kumzuia na kama wangelikuwa wanaweaza wangeliizuia Israel kipindi ilipokuwa imeundwa, kutokana na dhuluma zake. Wasomaji wote hawa wa Qur’an na wafanye ibada wote wameshindwa kumzuia Israel kutokana na dhuluma hizi. Hii ina maana zoezi la Saumu halikufaa. Saumu imekuja kuipa nguvu nia na utashi kiasi kwamba unaweza kumzuia yeyote ambaye anafanya dhuluma. Ulimwengu wa Kiislamu umeathirika na udhaifu wa nguvu ya utashi. Hawa wafanya ibada ni dhaifu zaidi katika nguvu ya utashi na nia. Katika mwezi huu, Imam Rahil (r.a) ameweka makini kwamba ikiwa umeimarisha nguvu ya utashi wako, basi njoo na usimamishe na kuwazuia maadui zako ambao wanajaribu kuudhulumu. Aliamrisha watu kutoka katika siku ya Quds ambayo imekuwa pia moja ya maadhimisho ambayo hufanyika Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani. Kama funga ya kila mtu ingekuwa imekuza nguvu yenu ya utashi. Lakini watu wengi walikataa wito huu kwa sababu tu umetolewa na kiongozi wa Kishia. Wakate wowote anacho kifanya Shia wafuasi wa Banu Umayyah hawatakifanya. Wafanye ibada wote hawa, na wafungaji saumu je watakuwa wamepotea na kama utataka kulithibitisha hili, futari haiwezi kuwa haijapotea, basi futari hazitaweza kuthibitisha hilo. Thamani ya kufunga kwako itakuwa na nguvu kiasi gani ili kuweza kuacha na kuwaachisha wengine. Huwa tunafanya maadhimisho ya siku ya Quds kila mwaka na mwaka huu inabeba ujumbe muhimu sana. Kama Hajj moja ya Ibrahim inatosha kutatua matatizo yote na ya umma mzima Imam Khomeini anasema katika kitabu chake kinachoitwa: Asrar Hajj ambapo tulielezea nguvu ya Hijja. Nguvu hiyo hiyo ipo ndani ya Ramadhani. Kwa ajili ya kuthibitisha kabla ya Eid kwamba nimefunga funga sahihi.
Siku hizi katika cricket na PSL vimechukua nafasi ambapo walikuwa wakifadhiliwa na wafanya biashara, na makampuni yaliyokuwa yakiisaidia PSL yalikuwa ni makampuni ya Kizayuni. Siku ya kwanza mmoja wa watazamaji alinyanyua bendera ya Palestina na akazuiliwa. Katika kipindi chote cha mashindano haikuonekana tena bendera ya Palestina haikuonekana tena kwa sababu wadhamini wake walidhibiti. Baadhi ya waandishi wa Habari waliweka pingamizi juu ya hili na kulikuwa na shiinikizo katika ligi hii. Pindi mashambulizi dhidi ya Palestina yalipoanza, matamasha ya miziki yalianza katika ngome ya Shahi wa Lahore kwa muda wa mwezi mzima. Pindi shinikizo lilipokuja , timu ya mwisho ambayo iliibuka mshindi walichukua bendera ya Palestina uwanjani na kuonyesha kwamba wao wapo na Wapalestina. Msako wote huu ulifanywa ili kuonyesha ni kwa kiasi gani wanafanya ili kuipa nguvu Israel. Hakuna kikwazo chochote kuhusu bendera ya Palestina nje ya uwanja , msikitini, Madrasa nyumbani kwako. Inabidi tuondoe uchafu huu. Ni siku 170 zimepita hadi sasa na kuna jinai zinaendelea kimya. Inabidi tuombe msamaha kwa hili. Sasahivi toba ya kivitendo kuanzia sasahivi hadi siku ya Quds ni kupamba Barabara zote kwa bendera ya Palestina. Inabidi sisi sote tutoke na kuelezea mshikamano wetu na kuunga mkono kwetu Wapalestina siku hiyo. Hakuna mtu anatakiwa kubaki nyumbani. Inabidi tuonyeshe kwamba Ramadhani imeamsha hisia , Uislamu na Qur’an. Inatakiwa tuanze harakati leo na kilele chake iwe ni siku ya Quds na baada ya siku hiyo tufanye kila liwezekanalo kwa ajili ya Palestina