EACO yajidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dk Jabiri Bakari (wa pili kutoka kushoto) akiwasilisha hoja kwenye kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) kilichofanyika Bububu, Zanzibar; wengine pichani ni Mtendaji Mkuu wa EACO Dkt. Ally Simba (wa kwanza-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo (wa kwanza kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano-Kenya Ezra Chiloba.

Zanzibar. Kamati-tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO) imejidhatiti kukuza sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki.
Mtendaji Mkuu wa EACO, Dk Ally Simba alisema wamedhamiria kuhakikisha wanakuza mahusiano katika mashirika katika taasisi wanachama ili kuwepo usimamizi mzuri wa huduma za mawasiliano.
“Tumedhamiria kuhakikisha mashirikiano baina ya taasisi zetu yanaimarika ili tukuze usimamizi thabiti wa huduma za mawasiliano katika nchi wanachama” alisema Simba.
EACO imeweka mkakati huo kwenye kikao kazi cha kamati hiyo kilichoketi, Bububu, Zanzibar mapema wiki hii.
Kikao kazi cha Kamati hiyo inayoundwa na Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano za Afrika Mashariki kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano  Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya, Ezra Chiloba; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano -Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo; Mtendaji Mkuu wa EACO Mtanzania Dk. Ally Simba; na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Rwanda, Deo Muvunyi.

Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Mawasiliano Afrika Mashariki (walioketi) na wataalam wa mawasiliano kutoka Mamlaka za Usimamizi wa mawasiliano Afrika Mashariki katika picha ya pamoja pembezoni mwa kikao-kazi cha Kamati-Tendaji ya Umoja wa Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO-Exco); walioketi kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani-Kusini, Elijah Alier Gai; Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usimamizi wa Mawasiliano-Burundi, Samuel Muhizi; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania -(TCRA) Dk Jabiri Bakari; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano na Matumizi ya Mawasiliano-Rwanda Deo Muvunyi; Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Mawasiliano-Uganda, Irene Kaggwa Sewankambo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Ezra Chiloba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Sudani Kusini, Napoleon Adok Gai. Mkutano huo ulijadili masuala ya usimamizi wa mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

EACO ilianzishwa mwaka 2012, kama muungano wa kikanda wenye sura ya kimataifa na kikanda ukilenga kuwaleta pamoja wasimamizi wa mawasiliano na wadau wa sekta ya mawasiliano Afrika Mashariki kwa shabaha ya kuboresha usimamizi na utoaji huduma za mawasiliano kwa wananchi wa Afrika Mashariki.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *