Ethiopia: Israel imewatorosha watu waliofanya mauaji katika jimbo la Tigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia amefichua kwamba, watu walioondolewa nchini humo na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa anwani kuwa ni Wayahudi walikuwa miongoni mwa wahalifu waliofanya mauaji katika eneo la Tigray.

Faraan: Abiy Ahmed ameyasema katika katika mazungumzo yake ya simu yasiyo ya kirafiki na mwenzake wa Israel, Naftali Bennett. Katika mazungumzo hayo Abiy Ahmed amekosoa hatua ya Israel ya kuwatorosha waasi na wahalifu waliotekeleza mauaji dhidi ya raia huko Tigray na kuwapelekea katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu ya Palestiina kwa kisingizio kwamba ni jamii ya Wayahudi waliowachache.

Ripoti zinasema Waziri Mkuu wa Ethiopia aliyekuwa akizungumza kwa hasira amemwambia Naftali Bennett kwamba, baina ya watu waliohamishiwa Israel wamo waliohusika na mauaji ya raia wa Tigray na kwamba wanapaswa kufikishwa mahakamani nchini Ethiopia.

Televisheni ya Israel imewanukuu maafisa usalama wakikiri kuwa, kwa uchache maafisa wanne waliohamishiwa Israel mwaka jana wanashukiwa kwamba walihusika na mauaji ya Tigray.

Awali gazeti la Haaretz la Israel lilikuwa limefichua kwamba, makumi ya Waethiopia waliohamishiwa katika utawala huo haramu kupitia operesheini ya siri katika kipindi cha utawala wa Benjamin Netanyahu wakitokea Tigray, si wafuasi wa dini ya Uyahudi.

Wakati wa utawala wa Benjamin Netanyahu, Wayahudi elfu mbili wa Ethiopia (mafalasha) walihamishiwa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Kwa sasa idadi ya mafalasha waliohamishiwa katika ardhi zilizoghusubiwa ambao pia ni mashuhuri kwa uhasama wao mkali dhidi ya Wapalestina, imezidi watu laki moja na elfu 40.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *