Ethiopia yaanza siku 3 za maombolezo baada ya maporomoko ya udongo kuua 260

Bunge la Ethiopia limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumamosi kufuatia maporomoko ya udongo yaliyoua mamia ya watu.

Taarifa rasmi ya Bunge la Wawakilishi la Ethiopia imeeleza kuwa, katika siku tatu hizo za maombolezo ya kitaifa, bendera zitapepea nusu mlingoti kote nchini, na katika meli, balozi, balozi ndogo na ofisi za uwakilishi za nchi hiyo kote duniani.

Kadhalika Bunge la Wawakilishi la Ethiopia limezinyooshea mkono wa pole familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na janga hilo la kimaumbile lililosababisha vifo vingi mapema wiki hii.

Idadi ya watu walioaga dunia katika maporomoko hayo ya udongo yaliyolikumba eneo la Gofa lililko kusini mwa Ethiopia baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo inazidi kuongezeka ambapo takwimu za karibuni zinaonyesha kuwa, imepindukia 250.

Maporomoko ya ardhi hushuhudiwa wakati wa msimu wa mvua nchini Ethiopia, ambao ambapo mwaka huu msimu huo ulianza Julai na unatarajiwa kuendelea hadi katikati ya Septemba.

Juhudi za kuwatafuta waliofukiwa na udongo katika maporomoko ya ardhi nchini Ethiopiia zinaendelea, huku matumaini ya kuwapata wakiwa hai yakizidi kupungua.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imethibitisha kuwa, watu 257 wamepoteza maisha katika janga hilo la kimaumbile huku ikionya kuwa, yumkini idadi hiyo ikapindukia 500.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *