Fikra ya kuangamizwa kwa Israeli; Demokrasia dhidi ya Demokrasia

Faraan: Wataalamu wakuu wa Palestina na Israel, pamoja na wanadiplomasia na wanasayansi wa kimataifa, wanajibu swali hili kwa kuchunguza hali ya miundo miwili ya serikali inayofana iliyofunika Bahari ya Mediterania nzima na Mto Yordani. Usanifu kama huo wa kisiasa ungebadilisha kabisa asili na hatari ya mzozo wa Israeli na Palestina, kuwazuia Waisraeli kukaa Ukingo wa Magharibi na kudumisha msimamo salama, na kuwaruhusu Wapalestina kukaa katika Palestina ya kihistoria na kuifanya Yerusalemu kuwa mji mkuu wao.

Siku ya Ijumaa tarehe 24 Mwezi wa nane kulingana na taqwimu ya Kiajemi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi alipokua akiwahutubia wageni wa Kongamano la thelathini na tatu la Umoja wa Kiislamu linalonasibishwa na mnasaba wa kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitangaza ya kwamba:

“Kutoa mwito wa kuangamizwa kwa Israeli haimaanishi kuangamia kwa Wayahudi. “Hii ina maana kwamba watu wa Palestina, ima wawe Waislamu, Wakristo au Wayahudi, lazima wachague serikali yao wenyewe.”

Amesisitiza kuwa Iran inapozungumzia uangamizaji wa utawala wa Israeli haimaanishi kuuawa kwa Wayahudi wa Israeli. Aliongeza kwa kusema: “Inamaanisha kuuangamiza utawala uliopo wa Kizayuni. “Uangamizaji wa Israeli unamaanisha kwamba watu wa Palestina, ima wawe Waislamu, Wakristo au Wayahudi, lazima wawe na uwezo wa kuamua hatima yao wenyewe na kuwaondoa majambazi mfano wa Netanyahu.”

Siasa rasmi iliyotangazwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwamba serikali hii ipo dhidi ya utawala wa Kizayuni, hivyo inasisitiza kwa uwazi kabisa kuangamizwa kwa Israeli.Hivi sasa Swali linakuja kwamba, ni nini maana ya fikra ya Jamhuri ya Kiislamu kuhusiana na kuangamizwa kwa Israeli? Maadui wa nchi ya Iran na utawala wa Kizayuni wanamaelezo yapi kuhusina na mtazamo huu wa Jamhuri ya Kiislamu? Je, uelewa wa Jamhuri ya Kiislamu juu ya suala hili ni tofauti na wengine au wote wanashirikiana katika uelewa huu?

Kaizari wa vyombo vya habari vya Magharibi, kwa kuzingatia sera zake za chuki na chuki aliyonayo dhidi ya Uislamu, ametoa wito mkali, wito wakivita na wakijeshi kwa ajili ya sera hii ya Jamhuri ya Kiislamu ; Na kwamba Iran inatafuta kampeni ya kijeshi dhidi ya Israel ili kutimiza kauli ya mwanzilishi wa mapinduzi kwamba Israel lazima iangamizwe. Hata hivyo, Kiongozi Muadhamu amesisitiza na kueleza kwa bayana kuhusu stratijia yenye misingi na ya kudumu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kwamba, kuangamizwa kwa Israeli inamaanisha kuangamizwa kwa mfumo wa kisiasa kwa ujumla, na kwamba ni ukoloni na unyakuzi wa Israeli ambao hauwapi Wapalestina nafasi ya maisha. Palestina ni ya Wapalestina wote; Ima Wawe Waislamu au Wayahudi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *