Filamu ya Montana; moja kwa moja inalenga kutangaza na kukuza ushoga wa kike

Faraan: Montana ni filamu iliyotengenezwa chini ya uongozi wa mkurugenzi wa Kiisraeli aitwaye Limor Shmila, iliyotolewa mwaka wa 2017. Miongoni mwa filamu nyengine zilizoongozwa na mkurugenzi huyu, ni kama vile “Time to Go” iliyotayarishwa mwaka wa 2016. Shmila, ambaye ni mwandishi wa filamu hiyo, alionyesha uhusiano wa kihisia na wa kingono kati ya wanawake hao wawili, hii ikiwa ni mada kuu katika kazi hiyo. Filamu hiyo yenye dakika sabini na tisa – 79 ilirekodiwa katika Maeneo maalum yaliyokua yamehifadhiwa na Lugha yake rasmi ni Kiebrania.

Muhtasari wa Filamu
Hadithi ya filamu inaanzia pale ambapo mhusika mkuu wa filamu hio anayefahamika kama Effi, alimpoteza babu yake na kurejea katika mji wake wa Acre baada ya kuishi nje ya mji huo katika maeneo yenye ardhi zilizochukuliwa kwa miaka 15. Hakuna maelezo mahususi yanayotolewa wakati wa filamu kuhusu siku za nyuma katika hadithi ya Effi.

Mara tu anaporudi katika mji wake, Effi alikutana na bibi yake, shangazi na mjomba wake, na kisha baadae anakutana na Jirani aliyekaribu na nyumba ya babu yake ambaye ni msichana anayeitwa Karen. Karen ni msichana aliyeolewa na ana binti mdogo anayeitwa “Maya” ambao wanaishi pamoja.
Uhusiano wa Karen na Effi polepole unakuwa wa karibu sana kiasi kwamba Effi anaamua kutumia muda mwingi mjini Acre akiwa Pamoja na Karen; Ukaribu huu ulimsababisha Effi kuwa mraibu wa Karen, na uhusiano wao wa kihisia ukabadilika na kuwa uhusiano usio wa kawaida, ukawa uhusiano wa kingono. Kadiri muda ulivyosonga na wanawake hao wawili wakizidi kubobea katika uhusiano wao, Effi aligundua ya kwamba Maya, ambaye ni binti yake Karen aliyekua na umri wa miaka tisa, ana ada ya kwenda kwenye nyumba ya Yosi ambaye ni mjombake Effi,matembezi haya yakiwa ni ya kisiri na yenye kutia shaka;
Effi analijadili swala hili pamoja na Karen, ingawaje ilikua vigumu kwa Karen kuamini uhusiano huu, na ikapelekea uhusiano wa Karen na Effi kuwa baridi na wenye misukosuko.

Suala kuu la filamu
Japokuwa, hadithi hiyo inaashiria ukosefu wa maadili na hatari ya uhusiano kati ya mwanamme na msichana mdogo mwenye umri wa miaka tisa, ila katika undani wa filamu hiyo, mwongozaji anaashiria “ushoga wa kike” na kudhihirisha uhusiano wa mwanamume na msichana mdogo zikiwa kama mfano wa matatizo na shida za kijamii. Inaonyesha kua uhusiano wa kimapenzi baina ya wanawake wawili ni jambo la kawaida na kwamba uwepo wake ni kitu cha kawaida yaani kisichokua na shida yeyote.

Tuzo
Filamu ya Montana ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika Tamasha la Kimataifa la Filamu la Toronto na tangu wakati huo imeonyeshwa katika maadhimisho yafuatayo:
Ameteuliwa katika Tuzo za ‘Ofiri’, miongoni mwa tuzo muhimu zaidi katika mrengo wa filamu za Israeli, katika kitengo cha Mwigizaji Bora Anayesaidia
Aliteuliwa katika Tuzo za ‘Ofiri’ kama Mkurugenzi Bora
‘Noa Biron’, mwigizaji katika nafasi ya Effi: Mshindi wa Tuzo ya Muigizaji Bora katika “Tamasha la Kimataifa la Filamu la Haifa”
Kuonyeshwa kwa filamu hiyo kwenye Tamasha la Filamu la Toronto na kuteuliwa kwa filamu katika kategoria mbili tofauti kwa tuzo ya “Ophir” kunaonyesha umuhimu wa filamu za ushoga kwa sinema za Magharibi na Israeli.

Vyanzo:
https://www.rogerebert.com/festivals-and-awards/tiff-2017-montana-kissing-candice-waru

TIFF 2017 Women Directors: Meet Limor Shmila — “Montana”


https://www.afterellen.com/movies/reviews/559615-montana-brings-a-quiet-message-about-resiliency

Montana [2017]: ‘TIFF’ Review


https://www.imdb.com/title/tt5261190/

[1]. Montana

[2]. Limor Shmila

[3]. ‘Time To Go’

[4]. Effi

[5]. Acre

[6]. Karen

[7]. Maya

[8]. Yossi

[9]. ‘Toronto International Film Festival ‘ – Tamasha la Kimataifa la Filamu la Toronto

[10]. Ophir Award

[11]. Noa Biron

[12]. ‘ Haifa International Film Festiva ‘ – Tamasha la Kimataifa la Filamu la Haifa

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *