Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan
Hotuba ya Ijumaa – 7 June, 2024
Hotuba ya1: Mama wa Taqwa zote ni mfumo wa kisiasa wa kiungu kuubadilisha mfumo wa na mifumo mingine ni dhihaka
Hotuba ya 2: Hamas imeanza vita ambayo haitaisha mpaka Israel itakapo tokomezwa.
Maisha mamoja ya mwanadamu ni ya kisiasa ambayo pia ni sehemu ya maisha ya kijamii ya mwanadamu ambayo ni sehemu kuu ya maisha ya mwanadamu. Maisha ya mtu binafsi ya mwanadamu ni kama kijusi kinachokuzwa ndani ya mwili wa mama ambayo ni sawa na jamii. Mtoto atabaki kuwa hai tu ikiwa mama atabaki kuwa hai. Utu wake utakuwa ni matokeo ya kile kinacho endelea ndani ya jamii hiyo kama ilivyokuwa kwa mama na mtoto, itakuwa hivyo tu. Kama jamii imeharibika basi na watu binafsi watakuwa wameharibika pia. Hii sio ambayo katika jamii gonjwa kuweze kulelewa na kukuzwa watu wenye afya.
Sheria hiyo hiyo inatumika katika ulinzi wa maisha na vilevile ambapo maisha ya mtu binafsi yamo katika mstari wa maisha ya kijamii, hivyo basi kama jamii imelindwa na ipo salama basi mtu binafsi pia atalindwa. Jamii ambayo ni uwanja mkubwa sio sehemu ya dini na katika taifa letu hata katika sayansi sosholojia haipewi umuhimu. Tumeachana na kutelekeza ugonjwa wa kijamii, utambuzi na matibabu ya maswala ya kijamii. Kila mtu amezingatia na kushughulikia zaidi maisha yake binafsi.
Mwelekeo wa kisiasa wa jamii ni moja wapo ya mambo ya msingi ikilinganishwa na nyanja fulani za kijamii ambazo ni za daraja la pili. Katika akili zetu dhana zote za kidini na za Qur’an zimepotoshwa kwa sababu tunaenda tu na maana zinazovuma. Tukimuuliza mtu siasa ni nini, ina maana ya kwamba fanya jambo fulani kwa njia ya uongo, udanganyifu, unafiki au kutumia zana au mbinu yoyote kufikia lengo lako. Hii ndiyo maana potofu. Siasa maana yake ni kupanga, kusimamia, kupanga mambo ya kijamii; kutoa njia na nyenzo kwa jamii, kulinda rasilimali, kugawa majukumu. Kama mtu ambaye ametengeneza kampuni na kuiendesha hiyo ni siasa. Mwanasiasa ni yule anayesimamia asasi yoyote ya kijamii. Jina linalotumika kwa Maimamu ni “Saasatul ‘Ibad” maana yake ni kuwa wanasimamia waja wa Allah.
Sehemu kubwa ya maisha ni ya kijamii na ndani ya siasa hiyo ndio kipengele kikuu ambayo inamaanisha kuwa jamii inahitaji hii kwanza. Kuendeleza jamii, kutoa njia zote muhimu za uchumi, elimu na kisha kudhibiti ufisadi katika rasilimali hizi, kutetea taifa na usimamizi wa mambo mengine ya jamii ni siasa. Imam Khomeini (r.a) alijifunza siasa kutoka kwa Syed Hassan Modarres aliyekuwa Najaf, kisha akaja Iran na kuanza kutoa miongozo ya kisiasa kwa watu. Alikuwa kielelezo cha Imam Khomeini (r.a) na Imam (r.a) alivutiwa naye. Modarres ndiye aliyesema mara ya kwanza kuwa Dini yetu ni siasa na siasa ni Dini. Nchini Pakistani dini ina maana ya ibada, maadili ya mtu binafsi na hakuna kitu cha kufanya katika jamii ambacho Iqbal anasema ni urithi. Dini hii inahusu tu kufikia mambo ya kiroho kwa mtu binafsi na haina uhusiano wowote na uchumi, maendeleo, siasa na kitu kingine chochote katika jamii. Imamu Khomeini (r.a) aliita fikra hii kama Tahajjur (iliyotuama kama jabali). Huu ni mtazamo finyu ambao hauna uhusiano wowote na jamii. Dini na mwakilishi wake ambaye ni Walii anawajibika kutoa elimu, njia za kiuchumi kwa jamii lakini katika dini ya Mutahhajjir hakuna jukumu wala wajibu.
Leo hii kila mtu ulimwenguni anafanya hivyo, na hii ndiyo sababu tunapenda jamii za Magharibi kwa sababu jamii yao imepangwa na kusimamiwa kisiasa. Hawajachukua kutoka kwenye dini lakini kulingana na masomo yao wenyewe na uzoefu wameendeleza na kupanga mambo ya kijamii. Huu ni uwanja halisi na sasa tunapaswa kufikiria kama Mwenyezi Mungu aliwapa Mitume imani tu na kukabidhi siasa ambazo ni uchumi, elimu, ulinzi kwa Firauni. Mwenyezi Mungu alikabidhi usimamizi wa mambo yote ya watu mikononi mwa Mtume. Maana ya Uimamu imeelezwa na Maimam wote kama usimamizi wa watu. Mwenyezi Mungu amewaweka Maimamu kwa ajili ya usimamizi na kuweka mpangilio wa jamii. Kwa vile umeondoa muongozo katika jamii basi hakuna siasa na hivyo bila ya Imamu, sote tupo tunaota ndoto ya kwenda peponi. Unachofanya hapa matokeo yake yatakuja baadaye. Pepo ni yale maisha ambayo unayaishi chini ya mfumo wa kiungu.
Quran imewasilisha Taqwa, ambayo ni ulinzi makhsusi kwa uwanja huu wa kijamii.
Surah Maida,Aya ya 57
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِنْ قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِينَ {57}
Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini.
Taqwa iliyotolewa na kuwasilishwa hapa kama mama wa ulinzi wote. Ikiwa utaamua ni nani awe Walii wako (kiongozi, mwenye mamlaka) basi mambo yote yatakuwa rahisi. Hapa aya inasema kwamba unapaswa kuishi maisha yako chini ya Walii na kisha ni nani wengine wanaoweza kuwa Walii wameonyeshwa katika Aya hii isipokuwa Mwenyezi Mungu. Inahakikishwa kwamba utakuwa unatumia maisha yako chini ya Walii lakini unahitaji tu kuona ni Wilaya ya nani, ima iwe ya Mwenyezi Mungu au Firauni, Wafalme, kiongozi wa kidemokrasia au baadhi ya wapotovu. Lazima ulitambue hii kwenye ulimwengu huu. Hakuna mtu katika dunia hii ambaye anaishi maisha yake nje ya Wilaya ya Mwenyezi Mungu.
Kwa Ahlul Sunna wanavyuoni wao wameibadilisha Wilaya kuwa Ukhalifa lakini hawajaeleza Ukhalifa umetoka wapi asili yake na mitazamo yake mbalimbali katika masuala ya uongozi wa kisiasa. Khilafat ni nafasi ambayo hupatikana kama mrithi katika yoyote. Jinsi Khalifa anateuliwa au kutengenezwa haieleweki kama vile Makhalifa wote wanne wa Waislamu walifanywa kuwa makhalifa kwa namna tofauti. Khalifa wa kwanza alifanywa kuwa khalifa katika mkutano, Khalifa wa pili aliteuliwa na wa kwanza, Khalifa wa tatu alifanywa kuwa khalifa na kamati ya watu sita na Khalifa wa nne alifanywa kuwa khalifa kwa viapo vya utii wa watu. Kisha Imam Hassan (a.s.) pia alifanywa kwa utii wa watu. Baada ya haya Ukhalifa uliendelea hadi kwa Banu Umayyah na ukaingia kwenye urithi wakaanza kurithishana. Wale ambao wanaamini kuwa Ukhalifa ni mfumo wenu, hawashughulikii jinsi Khalifa anavyopatikana na jambo la msingi ni kuukubali tu ndivyo waliwafunza. Kwa hiyo, kwao ni kazi rahisi.
Kwa Shia kuna sera ambayo kwayo Walii anachaguliwa na sera hii pia inatoka kwa Mwenyezi Mungu na sio kupitia demokrasia. Mwenyezi Mungu aliamua kuutengeneza mfumo wa Wilaya na watu waliuvuka na kuukiuka kwa urahisi sana na kuitia kona dini na mifumo ya Mwenyezi Mungu. Huwezi kupindua sheria yoyote ya Pakistan kwa urahisi lakini mfumo wa Mwenyezi Mungu unaweza kutupwa nje kwa urahisi. Wale ambao hawana Taqwa Quran inasema katika Aya hii watamkubali mtu yeyote kama Walii na kiongozi wao. Fisk na Fujoor huanza pale mwanadamu anapokwenda kinyume na kinyume na mfumo wa Mwenyezi Mungu na kujitengenezea Walii wake. Ikiwa utachagua Mawalii kama hao, viongozi basi sala zozote, ibada unazofanya hazikutengenezei akhera yako. Huu ni msimu wa Hijja na watu wanaenda kuhiji na Imamu wa Kaaba amesema Gaza ni Fitnah. Hijja hii ni mfano bora wa kutokuwa na siasa ndani yake na hakuna ibada ya kiroho katika hili.
Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba utakuja wakati baadhi ya wtu wataenda Hija kwa ajili ya biashara, wengine kwa ajili ya burudani, wengine kwa ajili ya kupata cheo cha Hija. Hili linaweza kushuhudiwa leo na Ale Saud wamebadilisha Hijja kwa njia sawa na matakwa ya Waislamu. Hakuna Muislamu anayepinga kuwa Hijja hii sio ya kIbrahim, kiQur’ani. Hijja ambayo ndani yake hakuna ruhusa ya kuunga mkono wanaokandamizwa watu wa Palestina, kulaani Israeli na Amerika. Hijja ina maana ya kujitenga na Taghoot, na kama hii imesimamishwa katika Hijja basi hii ni burudani tu na si kitu kingine. Imam (a) alimuashiria Shibli na kusema kwamba hakuna Hija ila ni watu tu wanaotoka kwa ajili ya kujifurahisha na kupiga kelele. Hii ni kwa sababu Banu Umayyah walikuwa wanafanya Hajj. Lau kama Hajj ingekuwa ya kiIbrahim, basi mahujaji wangetangaza kujitenga na Banu Umayyah kwanza. Imamu Hussian (a) alivua Ihram yake siku ya Hijja ili kuonyesha kwamba hii si Hijja ya kimungu.
Mwongozo wa kimsingi wa dini ni wa kijamii na kisiasa. Ni kupitia Wilaya ndipo usimamizi wa jamii, uongozi na utawala unapaswa kufanyika. Shia katika kila nchi wanapaswa kujibu unaishi chini ya mfumo wa nani? Mawalii ( viongoozi wako ni akina nani? Msiwafanye ni walinzi ambao wameipuuza dini yenu. Je, umekubali mifumo ya nani sasa hivi kwa wakati huu?
Pindi wanapotajwa Ahlul Kitabu huwa tunawanyooshea kidole Mayahudi na Wakiristo, na kuwatoa Waislamu nje ya kuitwa Ahlul Kitabu ambapo sio sahihi. Inabidi tuelezee sifa za Ahlul Kitabu na makafiri kwamba hawafai kukubaliwa kuwa walinzi kwa sababu wameifanya dini kuwa kejeli. Hata kama Muislamu atafanya hivyo basi pia, hawawezi kukubaliwa kuwa mlezi. Mzaha mkubwa zaidi ni kuuondoa mfumo wa Mwenyezi Mungu kutoka sehemu yake na badala yake kuwaweka wasimamizi kwa kupitia kura za watu. Ufisadi mkubwa kabisa (Fasaad) ni kuuweka pembeni Uimamu, Maimamu na kama Imamu Zainul Abideen ambaye hata Mashia walimkandamiza. Watu wa Kufah walimpuuza na kutengeneza utawala wao wenyewe. Nyinyi ndio mnaleta changamoto kwa alichokiweka Mwenyezi Mungu, basi pamoja na kuwa na demokrasia mnasema sisi ni Waislamu. Mnasimama na wazinzi, walevi halafu mnasema sisi ni Waislamu. Ikiwa nyinyi ni waumini basi jipatieni Taqwa ambayo ni mfumo mama wa ulinzi ambao utalinda kila kitu chenu.
HOTUBA YA PILI
Leo ubinadamu umekwisha kwa sababu dini na kila mfumo, miamala ya maisha haiko kwenye msingi wa Taqwa badala yake ipo kwenye tamaa, madaraka, matamanio n.k. Kudhulumu au kuwa watazamaji wa dhulma ni maisha ya motoni. Mataifa ya Waislamu ni yenye kuhuzunisha zaidi kwa sababu kama wangeirekebisha Taqwa hata kwa kiasi fulani wasingeona siku hizi hasa katika Gaza na Palestina.
Mwenyezi Mungu anasema kupata Taqwa katika maisha ya kisiasa ambayo kwayo msiwafanye walinzi na wasimamizi wengine (walinzi) na imetajwa katika aya mbalimbali. Na cha kushangaza ni kwamba Waislamu wamewachagua kuwa viongozi wale tu ambao dini imewakataza kuwafanya viongozi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema msiruhusu utawala kuingia mikononi mwa Banu Umayyah, vile vile Yeye (s) alitaja kutowadhulumu kizazi chake na Waislamu walikiuka haya yote kwa njia mbaya zaidi. Waislamu wamechagua viongozi wa aina hiyo ambao Waislamu wanashuhudia kupitia kwao viongozi wa namna hiyo siku hizi. Kipengele cha kutelekezwa kwa Quran kimekuwa ndio wasimamizi wetu katika siasa, dini, jumuiya na makundi mengine yote. Wametufanya wanyonge sana na leo tuko katika hali hii kutokana na hili.
Ni miezi nane leo na bado dhuluma inaendelea ambayo kila mtu anaishuhudia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Baadhi inafanywa na Israel na wengine na kila tukio linashuhudiwa na kila mtu.
Ukali wa ukandamizaji na dhuluma juu ya Rafah ulikuwa kwamba hata Netanyahu alisema lilikuwa kosa baya sana. Shetani Amerika ambaye yuko nyuma ya fitina hii yote ambaye ni baba haramu wa Israil pia ameeleza kwamba ukandamizaji umevuka mipaka na unapaswa kukoma. Biden anasema hivi kwa ajili ya kampeni yake ya uchaguzi kwa sababu Trump anasema ikiwa nitakuwa Rais, nitasimamisha vita vya Gaza mara moja kwa sababu watu wa Amerika pia wanataka vita hii isimamshwe. Sasa wanacheza na saikolojia ya watu kuonyesha kuwa tunataka kukomesha uonevu huu. Wote wanasema lakini Waislamu, Waarabu, UAE, Uturuki, viongozi wa Pakistani hawajasema kwamba ukandamizaji huu umevuka mipaka yote. Tabia zote mbaya za Banu Umayah kuanzia kwa Muawiya hadi Marwan ukiondoa Umar ibn Adul Aziz zikiwekwa pamoja tabia hizi zote zinapatikana kwa Erdogan. Amekuwa msaidizi wa Israeli katika vita. Kwa mujibu wa wizara yake alikuwa sehemu ya vita hadi tarehe 27 Machi 2024 na wakati huo huo anatoa taarifa ujumbe kwa mataifa ya Kiislamu juu ya kusitisha vita. Dhamiri za watawala wa Kiislamu ni mbaya Zaidi kuliko madhalimu. Wanaweza kusitisha vita hii kwa urahisi sana lakini hakuna nia au hamu ya kufanya hivi. Ikiwa Norway imeikubali Palestina, wanathamini lakini wao wenyewe hawaikubali.
Alichosema Kiongozi Muadhamu mnamo tarehe 4 Juni katika kumbukumbu ya Imamu Khomeini (r.a) ni sahihi. Israel ingeweza kufanya chochote walichoweza kufanya kwa kuua watoto, wanawake lakini kufikia malengo mengine ya Israeli haikuweza kufikiwa hata kwa 1%. Hawakuweza kuimaliza Hamas; hawakuweza kuwakomboa mateka wao. Hamas ilishambulia Tel Aviv wiki iliyopita na kuwakamata wanajeshi wa Israel wengi zaidi kwenye mahandaki. Kiongozi huyo alisema kuwa mwisho wa Israeli umeanza na anasema Israeli itaangamizwa na watu dhaifu zaidi. Wapalestina wameonyesha muujiza kwa upinzani na upambanaji wao na kitu pekee ambacho hawakuweza kufanya ni kulinda maisha ya watu wao kwa sababu hawakuwa na mitambo na vifaa vya vita.
Kiongozi alisema kwamba nitazungumza juu ya kile watu wakubwa wa Amerika na Ulaya wamesema kwamba Israeli inakaribia mwisho na hakuna anayeweza kuiokoa. Wakati wao wenyewe wanasema na kuamini kwamba Israeli inaenda kuisha basi kwa nini Waislamu hawawezi kushiriki katika hili. Ninayaeleza haya kwa ikhlasi kwamba kama hutajitenga na Taghot na kupaza sauti yako kwa ajili ya Palestina basi hii sio Hijja. Ikiwa hii ni Hijja na hamuwezi kufanya nyinyi wenyewe, basi mahujaji wa Iran wanafanya hivi tarehe 9 Zilhajj huko Arafah. Tulifanya hivi tulipokwenda Hijja na kutangaza kujitenga kwetu na taghoti ndani ya mahema yetu. Hata kama mtu atakuzuieni basi mnapaswa kuifanya tena pia. Siku bora ya kujitenga kwa Waislamu ni siku ya Eid na Waislamu wote wanapaswa kuanza hii kutoka Eid na kuendelea hadi dhuluma kwa wanawake na watoto itakapomalizika. Unaweza kuendelea kupigana na Hamas. Gazeti la Marekani lilisema kuwa Hamas imeanza vita visivyoisha na Israel, na haitamalizika Israeli itakapo tokomezwa. Mwenyezi Mungu ataiangamiza Israeli kupitia mikono ya hawa waliodhulumiwa tu.