HAMAS: Jihadi na mapambano yataendelea hadi kitakapokombelewa Kibla cha Kwanza cha Waislamu

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetoa tamko rasmi na sambamba na mkono wake wa pole kufuatia kuuwa shahidi Khalid Mansour, mmoja wa makamanda wa Brigedi za Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad al Islami ya Palestina, imesema kuwa, mapambano yataendelea hadi utakapokombolewa Msikiti wa al Aqsa ambao ndicho Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Tamko la HAMAS limesema, tunatoa mkono wa pole kwa umma wa Kiarabu na Kiisamu na taifa la Palesina hususan harakati ya Jihad al Islami kwa kuuawa shahidi Khalid Said Mansour, kamanda wa eneo la kusini la Brigedi za Quds pamoja na wenzake kadhaa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, damu za mashahidi siku zote ni sawa na taa iliyojaa nuru inayowamulikia njia wanamapambano na kuzidisha hasira zetu kwa adui Mzayuni. Damu hiyo inazidisha tu azma na mori wetu wa kuendelea na jihadi hadi utakapokombolewa kikamilifu Msikiti wa al Aqsa na kufanikishwa malengo yetu makuu matukufu ya kuzikomboa ardhi za Palestina na kurejea kwenye ardhi zetu za asili na jadi.

Kabla ya hapo harakati ya Jihad al Islami ya Palestina ilikuwa imethibitisha kuwa kamanda wake wa eneo la kusini, Khalid Mansour ameuawa shahidi huko Rafah katika shambulio la ndege za kivita za Israel.

Khalid Mansour alikuwa pia mjumbe wa Baraza la Kijeshi la Jihad al Islami na mmoja wa waanzilishi la tawi la kijeshi la harakati hiyo katika miaka ya 80.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *