Hamas: Kuchomwa wakiwa hai wanajeshi wa Misri na utawala wa Israel kunadhihirisha dhati ya ukatili

Ikitoa radiamali yake kwa habari kuhusu kuchomwa wakiwa hai makumi ya wanajeshi wa Misri katika vita vya mwaka 1967; Harakati ya Muqawama ya Palestina (Hamas) imesema kitendo hicho kinadhihirisha dhati ya ukatili na kutenda jinai ya utawala wa Kizayuni.

Gazeti la Yediot Aharanoth wiki hii lilifichua kuwa, utawala wa Kizayuni baada ya kupita zaidi ya miaka 50, jeshi la utawala huo katika vita vya mwaka 1967 kati yake na nchi za Kiarabu lilizika miili 70 ya wanajeshi wa Misri katika kaburi moja la umati na kisha kujenga sehemu ya kuegeshea magari katika eneo lililopo kaburi hilo.

Kaburi hilo la umati liko katika bustani moja katika mji unaojulikana kwa jina la “Mini Israel” ambayo ni sehemu ya mapumziko; eneo ambalo utawala wa Kizayuni ulilikalia kwa mabavu katika vita hivyo na kusababisha wakazi wa vijiji vitatu maarufu katika eneo hilo kwa majina ya Emmaus, Yalu na al Majdal kuyahama makazi yao hayo.

Hazim Qassim Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa, kufichuliwa jinai hiyo iliyotekelezwa na jeshi ghasibu la Kizayuni katika vita vya mwaka 1967 ya kuwauwa kwa kuwachoma wakiwa hai makumi ya wanajeshi wa Misri, kumedhihirisha kiwango cha ugaidi na dhati ya kutenda ukatili inayotawala katika vitendo na hatua za jeshi la utawala huo katika vita vyote dhidi ya wananchi wa Palestina.

Gazeti la Yediot Aharanoth limemnukuu Ze’ev Bloch mwanajeshi Mzayuni ambaye alishiriki vita hivyo vya mwaka 1967 na kuandika: Miili ya wanajeshi 70 na hata makumi ya wanajeshi wengine walizikwa katika eneo hilo; na hakuna mtu yeyote aliyekuwa anafahamu juu ya suala hilo.  Wakati huo Bloch alikuwa katika eneo hilo na ametunza siri hii kwa miaka 55.

Vita vya siku 6 vilivyojiri mwaka 1967ambavyo vinajulikana pia kwa jina la al Naksa miongoni mwa Waarabu vilisababisha vifo vya Waarabu elfu 15 hadi 25, na vilianza tarehe 6 hadi tarehe 10 mwezi Juni mwaka 1967.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *