Hamas: Kutiwa nguvuni wanamuqawama kunakofanywa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina ni kuihudumia Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa radiamali kufuatia hatua ya idara za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina ya kuwatia nguvuni wanamuqawama na wanachama wa harakati hiyo katika Ukingo wa Magharibi na kusisitiza kuwa, kitendo hicho ni sawa na kuuhudumia utawala wa Kizayuni.

Uratibu wa masuala ya usalama umeanzishwa kati ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Kizayuni tangu kufikiwa mapatano ya Oslo mwaka 1993; ambapo mamlaka hiyo inayoongozwa na Mahmoud Abbas imekuwa na nafasi kuu katika kutiwa nguvuni Wapalestina katika miaka yote hiyo.

Harakati ya Hamas jana Jumanne ilitoa taarifa na kutangaza kuwa kuendelea kamatakamata ya kiholela ya kisiasa dhidi ya viongozi na makada wa harakati hiyo, mateka na wanaharakati walioachiwa huru ni siasa zililizofeli na kugonga mwamba.

Hamas imesisitiza kuwa, ukiukaji huo unadhihirisha kuendelea mashinikizo dhidi yake  kwa lengo la kufanikisha maslahi maalumu ambayo kwa upande mmoja yanahudumia mirengo yenye ushawishi ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala ghasibu wa Israel.

Hamas kwa mara nyingine tena imeyatolea wito makundo yote ya kiraia zikiwemo taasisi za haki za binadamu, kada za kisheria na mirengo mbalimbali kuchukau hatua za kuzuia kufanikishwa sera hizo za Israel na wakati huo kufanya juhudi ili kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa.

Duru za usalama za utawala za Kizayuni zimeeleza kuwa  zinatiwa wasiwasi na kuongezeka oparesheni za Wapalestina dhidi ya maeneo mbalimbali huko Israel  na kutahadharisha juu ya kupamba moto oparesheni hizo nje ya Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan katika miezi ijayo na kushtadi harakati za makundi ya muqawama ya Palestina dhidi ya Israel.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *