Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa maneva ya al Rakan al Shadid 3 yanayonesha nguvu ya muqawama.
Hazim Qassim Msemaji wa Hamas ameeleza kuwa, maneva ya Al Rakan al Shadid 3 yaliyofanywa na chumba cha oparesheni za pamoja kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza yametilia mkazo umhimu wa hatua za pamoja za makundi ya muqawama na mshikamano wao.
Msemaji wa Hamas amesisitiza pia kuhusu ulazia wa kuendeleza utendaji wa kimaidani na kuongeza kuwa maneva hayo ni ujumbe wa wazi kuhusu umoja wa wananchi wa Palestina.
Hazim Qassim ameongeza kuwa, maneva hayo yanatilia mkazo kuhusu kuwa tayari mirengo ya kijeshi ya makund ya muqawama kwa ajili ya kukabiliana na matukio yote huko Palestina na kujiandaa pia kwa ajili ya kuwalinda wananchi, matukufu, ardhi na familia za mashujaa khususan kukabiliana na serikali ijayo ya Kifashisti ya utawala ghasibu wa Kizayuni.
Chumba za oparesheni za pamoja za makundi ya muqawama ya Palestina jana yalitangaza kuendesha maneva kubwa ya kijeshi kwa jina la Al Rakan al Shadid 3 huko kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.