Hamas: Risasi za wanamapambano wa Palestina ni jibu kwa vitendo kwa jinai za Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema kuwa, risasi zilizopigwa na wapiganaji ukombozi wa Palestina katika operesheni ya kulipiza kisasi karibu na makazi haramu ya walowezi katika eneo la kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni jibu la kivitendo kwa jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Msemaji wa Hamas Hazem Qassem alisema katika taarifa yake kwamba operesheni ya Jumamosi usiku karibu na makazi haramu ya Israel ya Kiryat Arba, ambapo walowezi wa Kiisraeli aliuawa na watu wengine wanne kujeruhiwa, “inathibitisha kwamba mapambano yanaweza kuwashangaza wavamizi na kuwapa mapigo makali.”

Risasi za wanamuqawama (wanamapambano wa Kiislamu) ni jibu la kivitendo kwa sera za upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni, jinai wanazofanya, na kuvunjia heshima kwao mara kwa mara eneo la Msikiti wa al-Aqsa na Msikiti wa Ibrahim,” alisisitiza.

Zaidi ya hayo, chama cha Popular Front for the Liberation of Palestine (PFLP) pia kilisema kwamba operesheni hiyo ya ufyatuaji risasi inaashiria kuwa roho ya muqawama inazidi kuongezeka miongoni mwa Wapalestina na inaonyesha kuwa mapambazuko ya mapinduzi ya wananchi na wakati sasa umewadia wa ukombozi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Makundi ya muqawama wa Palestina yamepongeza operesheni ya wanamapambano wa Kipalestina katika mji wa al Khalil huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza udharura wa kuendelezwa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wakisema, utawala huo hauelewi isipokuwa lugha ya mabavu.

Ni baada ya operesheni iliyotekelezwa na mpiganaji wa Kipalestina “Mohammed Kamal al-Ja’bari” katika mji wa al Khalil ulioko kusini mwa Ukingo wa Magharibi, ambapo Mzayuni mmoja aliuawa na wengine 5 kujeruhiwa.

Vyombo vya habari vimesema al-Jabari ni mpiganaji wa kundi la Hamas, ambaye kaka yake Wael alikuwa akitumikia maisha katika jela ya Israel kabla ya kuachiliwa na kupelekwa Ukanda wa Gaza katika mkataba wa kubadilishana wafungwa wa Gilad Shalit mwaka 2011.

Vikosi vya Israel hivi karibuni vimekuwa vikiendesha mashambulizi na mauaji kila siku katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, hasa katika miji ya Jenin na Nablus, ambako makundi mapya ya wapiganaji wa muqawama wa Palestina yameundwa.

Wizara ya Afya ya Palestina ilisema katika ripoti yake mpya jana kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel umewauwa shahidi takriban Wapalestina 183 tangu mwanzoni mwa 2022 katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza unaokaliwa kwa mabavu, wakiwemo 26 tangu mwanzoni mwa Oktoba.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *