Harakati ya Hamas ilitangaza kuwa uwongo wa msemaji huyo wa adui Mzayuni ni ishara ya uamuzi wa utawala huo wa kufanya jinai nyingine dhidi ya Wapalestina, hali ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi kuliko jinai ya hospitali ya al-Mu’amdani.
Hamas ilisema: Zaidi ya Wapalestina 40,000 walikimbilia katika Hospitali ya al-Shafa. Tunatahadharisha kuhusu mauaji mapya na tunatoa wito kwa viongozi wa dunia kuchukua hatua ili kuyazuia yasitokee tena.
Msemaji wa Hamas aidha ameeleza kuwa, adui Mzayuni anajaribu kuinua ari ya jeshi lake kwa kuwasilisha riwaya ya uwongo na kusisitiza kuwa viongozi wa Hamas wapo majumbani mwao na sio hospitalini.
Hapo awali msemaji wa jeshi la utawala huo ghasibu alidai kuwa makao makuu ya Hamas yapo chini ya hospitali ya al-Shafa huko Gaza.
Zaidi ya hayo, msemaji wa Hamas alisema: Matangazo haya ni ya upotoshaji na ya uwongo na viongozi wote wa Hamas wako majumbani mwao na sio mahospitalini.
Mwanachama wa vuguvugu la Hamas ameongeza kuwa: Utawala unaokalia kwa mabavu unalenga watoto na wanawake, na upinzani unaendelea kudhibiti vita kwa nguvu zake zote.
Msemaji wa Hamas alisema: Jeshi la Israel linaharibu miundo mbinu ya Ukanda wa Gaza, hususan nyumba na hospitali.