Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilithibitisha rasmi kuuawa shahidi Yahya Sanwar, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati hio.
“Khalil al-Hayya”, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, mchana wa leo (Ijumaa), katika ujumbe uliotangazwa kwenye mtandao wa “Al-Aqsa”, alithibitisha rasmi kuuawa shahidi “Yahya Al-Sinwar” , aliyekua mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas.
Hapo jana, jeshi la Israel lilitangaza katika taarifa yake kwamba wanajeshi wa utawala huo walimuua Kiongozi huyo, japo haikua katika operesheni iliyopangwa awali, ingawaje wakiwa katika hali ya mapambano na makundi ya muqawama ya Palestina katika eneo la “Tal al-Sultan” lilopo kusini mwa Ukanda wa Gaza walikuatana na Bw. Sinwar pasi nakutarajia.
Kinyume na madai ya hapo awali ya utawala wa Kizayuni kuhusu Sinwar kuwatumia wafungwa kama ngao za binadamu, “Golgetz” wa redio ya jeshi la Israel alitangaza kuwa, Yahya al-Sinwar aliuawa shahidi akiwa amevalia sare za kijeshi na kupigana mstari wa mbele na askari wa Israel.
Khalil al-Hayya, ambaye ni mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, alianza kwa kutoa pole na rambirambi kwa kuuawa kishahidi Al-Sinwar na kisha akasisitiza kwamba damu yake itakuwa mwanga kwa vikosi vya upinzani na itawapa motisha zaidi na utulivu katika njia hii.
Vilevile Al-Hayya alisema kuwa Hamas itaendelea na juhudi zake za kuanzisha taifa la Palestina na mji mkuu wa Jerusalem.
Wakati huo huo, afisa huyo mkuu wa Hamas akisisitiza kwamba kuuawa shahidi Yahya al-Sanwar na viongozi wengine wakuu wa Hamas kutaongeza motisha na nguvu za makundi ya upinzani.
Khalil al-Hayya alitangaza kuwa, wafungwa wa utawala ghasibu wa Kizayuni watarejea pindi tu uvamizi wa Ukanda wa Ghaza utakaposimama, wanajeshi wa Israel watajiondoa kikamilifu katika Ukanda wa Ghaza na hatimaye wafungwa wa Kipalestina kuachiwa huru.