Hassan Sheikh Mahmoud ateuliwa kuwa rais mpya wa Somalia

Bunge na seneti ya Somalia zimemchagua rais wa zamani Bw. Hassan Sheikh Mahmoud kuwa rais wa nchi hiyo kwa muhula wa miaka minne.

Vyanzo vya habari viliripoti ushindi wa Rais wa zamani wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud uliopatikana kupitia uchaguzi wa bunge na kufanikiwa kua raisi kwa muhula wa miaka minne.

Alikuwa rais wa nane wa Somalia kuingia mamlakani nchini Somalia mnamo Septemba 16, 2012 na kumrithi Sharif Sheikh Ahmed. Kisha katika duru iliyofuata, mnamo Februari 8, 2017, katika uchaguzi wa rais wa Somalia, alishindwa na Mohammad Abdullah Mohammed.

AFP iliandika kuwa, Hassan Sheikh Mahmoud alishinda kiti cha urais kwa mara ya pili huku kukiwa na hali ya wasiwasi nchini Somalia na tishio la njaa, huku wabunge na baraza la Seneti la Somalia wakimpigia kura.

Baraza la Wawakilishi la Somalia lenye wajumbe 275 na Seneti yenye wajumbe 54 wanamchagua Rais mpya wa Somalia. Uchaguzi huu uliahirishwa hadi duru ya pili, kwani hakuna mgombeaji hata mmoja aliyeshinda theluthi mbili ya kura katika duru ya kwanza.

Katika awamu ya kwanza ya upigaji kura, miongoni mwa kura 329, Rais wa Pantland Saeed Abdullah Dani alipata kura 65, Rais Mohamed Abdullah Fumako kura 61, Rais wa zamani wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud kura 52 na Waziri Mkuu wa zamani Hassan Ali Kheiri kura 48.

Kulingana na ripoti ya AFP, siku ya Jumapili Mei 15, baada ya uchaguzi wenye kusisimua kufanyika ambapo wagombea 36 walichuana na habari za matukio hayo kutangazwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa, rais wa zamani wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud alipata kura 165 za wabunge, zaidi ya idadi inayohitajika kushinda dhidi ya Rais wa Somalia Mohammed Abdullah Mohammed.

Hapo awali, wachunguzi wa masuala ya kisiasa na wachambuzi walisema kwamba kuchaguliwa tena kwa Mohammed Abdullah Mohammed haingewezekana kutokana na kutokuwepo kwa washirika wao katika nafasi za juu bungeni, na Sharif Sheikh Ahmed na Hassan Sheikh Mahmoud, marais hawa wawili wa zamani wa Somalia, walisemekana kuwa na nafasi nzuri ya kugombea urais.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *