Mvutano kati ya Morocco na Algeria umeongezeka tangu ziara ya hivi majuzi ya Waziri wa Vita wa Israel Benny Gantz nchini Morocco na kutiwa saini mkataba wa ushirikiano wa kiusalama kati ya pande hizo mbili, kulingana na Shirika la Habari la Fars.
Gazeti la Kizayuni la “Jerusalem Post” lilijibu ripoti ya gazeti la Ufaransa la “Lupinion” kuhusu kushadidi mivutano kati ya Morocco na Algeria na kuandika kuwa mivutano hiyo inatokana na harakati za Israel katika eneo la Kaskazini mwa Afrika.
Gazeti la Jerusalem Post limeongeza kuwa, ziara ya hivi karibuni ya Bani Gantz nchini Morocco na kutiwa saini hati ya maelewano na mwenzake wa Morocco, hati ya kwanza ya maelewano kati ya utawala wa Kizayuni na Morocco, huenda kumeibua wasi wasi wa Algeria kuhusu kuongezeka ushirikiano kati ya Rabat na Tel Aviv.
Gazeti la Ufaransa la Lupineon pia limenukuu chanzo kimoja kikisema kuwa, mivutano kati ya Algeria na Morocco inazidi kuongezeka kila kukicha na kwamba hii leo kumezuka gumzo la vita kati ya nchi hizo mbili za eneo la Kaskazini mwa Afrika.
“Algeria haitaki vita na Maghreb, lakini iko tayari kwa vita,” kilisema chanzo kimoja cha habari katika jeshi la Algeria.
Kwa mujibu wa gazeti la Al-Quds Al-Arabi, duru hiyo imeongeza kuwa, kilichoikasirisha Algeria ni uungaji mkono wa Israel kwa Maghreb.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, silaha ambayo imewatia wasiwasi wananchi wa Algeria ni vita vya kielektroniki na ndege zisizo na rubani.
Kabla ya hapo, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kutiwa saini makubaliano ya kijeshi ya dola milioni 22 kati ya Morocco na sekta ya anga ya utawala wa Kizayuni kwa lengo la kuipatia Morocco ndege zisizo na rubani za “kamikaze”.
Hatua za Israel za kuongeza mvutano kati ya Algeria na Magharibi (Morocco)
