Hisia za Marekani kwa ziara ya Rais Bashar al-Assad ya Imarati

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alieleza maoni yake kuhusu ziara ya rais wa Syria katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kulingana na Huduma ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani katika mahojiano na Al Jazeera alijibu ziara ya Bashar al-Assad ya UAE.

“Tunasikitishwa na juhudi za uhalalishaji wa Rais Bashar al-Assad,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alinukuliwa akiyasema hayo na Al Jazeera.

Wakati wa ziara yake ya UAE siku ya Ijumaa, Bashar al-Assad alikutana na idadi ya maafisa wa UAE, akiwemo Gavana wa Dubai Mohammed bin Rashid Al Maktoum na Mwanamfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan.

Syria imekuwa uwanja wa mapigano makali tangu mwaka 2011 kati ya vikosi vya jeshi la Syria, makundi ya kigaidi na makundi yenye itikadi kali vita hivi vikiwa dhidi ya serikali kuu.

Ripoti nyingi zikiwemo za vyombo vya habari vya Magharibi, zinaonyesha kuwa nchi za Magharibi zimetoa msaada wa silaha, kijasusi na vifaa kwa makundi hayo kwa nia ya kuiangusha serikali ya Syria.

Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aliiambia Al Jazeera kuwa Bashar al-Assad ndiye aliyehusika na vifo vya Wasyria wengi. Alisema; “Wale wanaofikiria kujihusisha na utawala wa Assad wanapaswa kuzingatia uhalifu wake,”.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema Washington haitaondoa vikwazo dhidi ya Syria na haitaunga mkono ujenzi mpya hadi maendeleo yatakapopatikana katika mchakato wa kisiasa nchini Syria.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *