Hizbullah yathibitisha mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah ameuawa shahidi katika hujuma ya kigaidi ya Israel

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa harakati hiyo, Sayyid Hassan Nasrullah, amuawa shahidi katika mashambulizi makubwa ya anga ya Israel yaliyolenga majengo ya makazi ya raia kusini mwa Beirut, jana Ijumaa.

Katika taarifa yake iliyotolewa alasiri ya leo Jumamosi, Hizbullah imesema: Sayyid wa Muqawama, mja mwema, amerejea kwa Mola wake akiwa shahidi mkubwa na kiongozi shupavu, shujaa na muumini wa kweli, akiungana na msafara wa nuru wa mashahidi wa Karbala katika njia ya Mwenyezi Mungu, na akifuata nyayo za Mitume na Maimamu waliouliwa shahidi,”

Taarifa hiyo ya Hizbullah imeongeza kuwa: Tunatoa mkono wa pole kwa Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Walii Amri wa Waislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, mujahidina, waumini, wanamuqawama, taifa letu lenye subira na Mujahid la Lebanon, Umma mzima la Kiislamu, wapigania uhuru wote na wanaodhulumiwa duniani, na vilevile kwa familia yake…”.

Hizbullah iimesema katika taarifa hiyo kwamba: Tunampongeza Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa kupokea nishani ya juu kabisa ya Mwenyezi Mungu, nishani ya Imam Hussein, amani ya Allah iwe juu yake, kwa kutimiza matamanio yake na kupata cheo cha juu zaidi cha imani na itikadi, akiuawa kama shahidi katika njia ya Quds na Palestina. Vilevile tunatuma rambirambi na baraka zetu kwa mashahidi wenzake waliojiunga na msafara wake safi na mtakatifu kufuatia hujuma ya kihaini wa Wazayuni kwenye viunga vya kusini mwa Beirut.”

Hizbullah imesisitiza katika taarifa hiyo kwamba: Uongozi wa Hizbullah unamuahidi shahidi wa juu zaidi, mtakatifu na wa thamani zaidi katika safari yetu iliyojaa mihanga na mashahidi, kuendeleza mapambano ya Jihadi katika kukabiliana na adui, kuiunga mkono Gaza na Palestina, na kuinda Lebanon na taifa lake imara na sharifu.

Tangu mchana wa jana Ijumaa, ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi zaidi ya 30, yakilenga majengo ya makazi ya raia huko Burj al-Barajneh, Kafaat, Choueifat, Hadath, al-Laylaki, na Mreijeh, mjini Beirut, huku vyombo vya habari vya ndani vikiripoti kwamba, zaidi ya watu 300 wameuawa kutokana na mashambulizi hayo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *