Shambulio la ‘Pagers’ lalenga ‘kuchochea vita kuu katika Mashariki ya Kati’: Urusi
“Tunachukulia kilichotokea kama kitendo kingine cha vita vya mseto dhidi ya Lebanon, ambacho kimedhuru maelfu ya watu wasio na hatia,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova alisema katika taarifa.
“Inaonekana kuwa waandaaji wa shambulio hili la kiteknolojia ya hali ya juu walikududia kuzua makabiliano makubwa ya silaha ili kuchochea vita kuu katika Mashariki ya Kati.”
Awali, wizara hiyo ilieleza kuwa uchunguzi ulihitajika kuhusiana na tukio hilo.