Baada ya misimamo ya Hollywood ya kuunga mkono watu wa Palestina, mwandishi na mchambuzi wa Marekani Belen Fernandez aliandika katika makala kwamba ni wakati tena kwa polisi wa imani wa Hollywood kuacha kutumikia kwa uaminifu utamaduni wa watu mashuhuri wa Marekani na kufanya wajibu wake wa kuthibitisha simulizi ya Kizayuni wakati huu wa vita ndani ya mji wa Gaza.
Wakati vita vya Israel dhidi ya Gaza vimeingia mwezi wake wa tatu, kumekua na pengo kubwa katika makampuni ya uzalishaji wa filamu na mashirika ya vipaji ya Hollywood, baada ya idadi kubwa ya waigizaji na watengenezaji filamu kuchukua misimamo dhidi ya mauaji ya Gaza na kuunga mkono watu wa Palestina.
Uwiano mpya na upeo wa uhusiano wa karibu kati ya Hollywood na Tel Aviv vimekuwa wazi zaidi.Fernandez, ambaye ameandika makala nyingi kwa New York Times, Al Jazeera na Middle East Eye, katika makala yake ya hivi punde iliyochapishwa kwenye tovuti ya kituo cha televisheni cha Al Jazeera, alichunguza majibu ya Hollywood kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza na uhusiano kati ya siasa na sinema.
Katika moja ya kesi ambazo zilizua kelele nyingi baada ya vita vya Gaza, Melissa Barrera, mwigizaji wa filamu “Scream”, amekataa kuendelea kufanya kazi na waundaji wa awamu mpya ya franchise hii ya kutisha kutokana na uchapishaji wa makala kwenye ukurasa wake wa kibinafsi katika mitandao ya kijamii akikosoa shambulio la Israel kwenye eneo lililozingirwa.
Jinai au kosa lake likiwa ni ombi la kusitishwa mapigano huko Ghaza na nukuu kutoka kwa mwanahistoria wa Israel, Rose Segal, ambaye alielezea mienendo ya hivi sasa ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina kuwa ni “ushahidi wa wazi wa mauaji ya halaiki”.
Kampuni ya Spyglass, inayohusika na kumtimua Barrera, ilidai kuwa kauli za mwigizaji huyo wa Mexico ni za chuki dhidi ya Wayahudi; Ingawa mwigizaji huyu ameomba tu kusitisha mizozo ambayo imesababisha vifo vya elfu kumi na nane hadi sasa na kunukuu sentensi kutoka kwa profesa wa masomo ya mauaji ya halaiki na mauaji katika Chuo Kikuu cha Stockton mjini ‘New Jersey’.
Katika ripoti yake kuhusu Barrera, Newsweek ililazimika kukiri kwamba “baadhi ya wakosoaji wa Uzayuni wanaamini kwamba kuundwa kwa Israel kuliwalazimisha Wapalestina kuondoka katika ardhi yao.” Katika suala la ujinga, hii ni sawa na kusema “Baadhi ya wakosoaji wa hali ya hio wanaamini kuwa vimbunga havipo.”
Kwa kuzingatia takwimu zinazoashiria kwamba kuanzishwa kwa Israel kulisababisha kuuawa kwa Wapalestina 10,000, kuharibiwa kwa vijiji 500, na watu 750,000 kuhama makazi yao, inaonekana kwamba Newsweek imepitisha mkakati wa Hollywood wa kupuuza ukosoaji wa Israel.
Barrera hakuwa nyota pekee wa Hollywood ambaye alikiuka maandishi ya Kizayuni. Mshindi wa tuzo ya Oscar Suzanne Sarandon aliachishwa kazi na wakala wa talanta UTEA kwa kushiriki katika maandamano ya wafuasi wa Palestina na kukosoa shambulio la bomu la Gaza. Mark Ruffalo, ambaye alilazimika kuomba radhi mwaka 2021 kwa kukosoa “mauaji ya halaiki” ya Israel katika Ukanda wa Gaza, alilengwa tena na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaotawaliwa na Wazayuni. Katika taarifa yake ya mwisho, alikosoa mateso ya watoto wa Palestina na Israel.
Kwa upande mwingine, waigizaji wengi mashuhuri wa Hollywood walionyesha mshikamano wao na Israel, ambayo ilipata kushindwa vibaya katika shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas.
Mwanzoni mwa vita, mshindi wa tuzo ya Oscar na Golden Globe, Jamie Lee Curtis, kwa kuweka picha ya watoto wa Kipalestina wanaokimbia mashambulizi ya Israel, alisema kimakosa kwamba watoto wa Israel walikuwa hatarini kwa mashambulizi ya kigaidi ya Wapalestina.
Malkia wa urembo wa Israel, Gol Gadot, ambaye aliigiza katika filamu ya “Wonder Woman”, aliandika maandishi yenye kuunga mkono mauaji ya Gaza kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema: “Nasimama pamoja na Israeli; Nanyi mnapaswa kuwa na msimamo kama huu.”
Gadot, ambaye ana mchango mkubwa sana katika kudhihirisha uhalali wa uvamizi wa Israel na kwamba aliyeunga mkono mauaji ya umati ya Wapalestina, alisifiwa na jarida la ‘Times’ mnamo mwaka 2018 kuwa mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani.
Vilevile Rais wa zamani wa Israel Reuven Rivlin alimtambulisha mwigizaji wa filamu ya “Red Notice” kama “balozi wa kweli na maarufu” wa Tel Aviv.
Mnamo mwaka wa 2017, Gadot alijifanya kama mwanajeshi wa kike wa Israeli kwa jarida la Maxim na akatoa matamshi yenye utata kuhusu “utakaso wa kikabila”. Picha hizi zilileta umaarufu na bahati nzuri kwa muigizaji huyu.
Picha ya Israeli kwenye skrini pia iliimarishwa mnamo 2022: wakati ‘Marvel Studios Disney’ ilitangaza kwamba kwenye sinema “Kapteni Amerika; “Dunia Mpya ya Jasiri” ina mhusika anayeitwa Sabra ambaye ni mwanachama wa Mossad.
Kwa hivyo, kwa nini Hollywood ina “tatizo la Israeli” kama hilo? Bila shaka, hakuna haja ya kutumia nadharia za njama kueleza na kufasiri mwelekeo wa tasnia ya filamu [ya Marekani] kuelekea hali ya ukandamizaji; Ni wazi kabisa kwamba uhusiano maalum wa Israel na Marekani unamaanisha kuwa kuitukuza Israel katika utamaduni maarufu kunatumikia moja kwa moja malengo ya sera za kigeni za Marekani.
Kampeni za propaganda ni zenye kudidimiza kiasi kwamba watu kama vile Paris Hilton na Kendall Jenner wanapoonyesha huruma kwa Palestina kwenye mitandao ya kijamii, machapisho yao hufufutwa kwa haraka.
Gigi na Bella Hadid ni miongoni mwa walengwa wengine wa Kizayuni ambao ni miongoni mwa watu mashuhuri kwa sababu ya uungaji mkono wao kwa Palestina. Baba mzazi wa wanamitindo hawa wawili maarufu, Muhammad Hadid, alizaliwa Palestina mnamo mwaka 1948. Naye Bella amepokea mara kwa mara ujumbe wa vitisho vya kuuawa kwa kudhihirisha msimamo wake kua yuko pamoja na Palestina. Mashine ya propaganda ya Israel imepotosha ukweli kiasi kwamba ombi la kusitisha mapigano limefanywa kuwa jambo lililodhidi ya sheria ikilinganishwa na uangamizaji wa wakazi wa Gaza.
Vilevile Akaunti rasmi ya serikali ya Israel imemkosoa JJ na kutafsiri ombi lake la amani kati ya Palestina na Israel kama ” hali ya kufumbia macho mauaji ya watoto wa Kiyahudi majumbani mwao”.
Kwa mujibu wa habari, hivi sasa watoto na watu wazima wa Kipalestina wanauawa kwa kiwango cha kutisha na jeshi la Israel, ambalo limezindua “apocalypse ya sinema” huko mjini Gaza, ni matarajio yetu ya kwamba nyota wa Hollywood na watu wengine mashuhuri hawatozama kabisa katika mahandaki ya Wazayuni. Japo kua kwa sasa, “Ukweli na haki” kamwe havitaonyeshwa kwenye sinema za siku zijazo.