Hotuba ya Ijumaa – 24 Juni 2022,  Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hotuba ya Ijumaa – 24 Juni 2022

 Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

 (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)

 Imetolewa: Msikiti wa Baitul ul Ateeq

 Lahore – Pakistan

 

 Hotuba ya 1:  Msiba wa mwanachuoni ni Kupenda Uongozi.

Ninawausieni nyinyi pamoja na kuiusia nafsi yangu katika kumcha Mwenyezi Mungu na nawasisitizieni  kuyasimamisha maisha yenu katika misingi ya (Taqwa) Uchaji Mungu. Ucha Mungu (Taqwa) ni mpango na mikakati kutoka kwa Mwenyezi Mungu yenye kumlinda mwanadamu anayopaswa kuitekeleza katika maisha yake.  Ni sifa kamilifu inayohifadhi ubinadamu, uwezo, na ni sifa inayopatikana katika kila sehemu ya maisha.  Ikiwa Taqwa itakosekana katika nyanja muhimu za maisha ya mwanadamu, basi mwanadamu huyu atakumbana na majanga makubwa. Kizazi cha sasa ni ushahidi wa ukweli huu, kwamba maisha yao bila ya Taqwa hasa kizazi cha Kiislamu licha ya kuwa na uhusiano na dini , licha ya kua pamoja na Seerah ya Bw. Mtume (s.a.w.w) na Quran ambayo ni kitabu cha uongofu ila bado maisha yao hayajasalimika kutokana na janga hili. Chanzo chake ni ukosefu wa Taqwa katika nyanja muhimu za maisha yetu.

Nyanja muhimu za maisha kwa kila mmoja wetu ni dini ambapo mwanadamu hutumia sehemu kubwa katika nyanja ya dini.  Sehemu ya pili ya maisha inayomhusu kila mmoja wetu  ni siasa.  Sehemu ya tatu ni uchumi (mbinu za maisha) na kuna nyanja nyenginezo chini ya hizi. Katika nyanja zote hizi ikiwa tutataka kushuhudia mandhari jinsi yalivyo bila ya Taqwa basi tunaweza kuitazama jamii yetu na kutathmini jinsi maisha yatakavyokua bila ya Taqwa na pia kutambua majanga yanayotokana na hali hii,  na vilevile vikwazo na ukosefu wa usalama mbele ya macho yetu.  Ukweli huu uko wazi kama mwanga wa Jua nchini mwetu.  Ikiwa Siasa itaenda bila ya Taqwa na uchumi ukawa kinyume na misingi ya Taqwa basi tusitarajie matokeo mengine kando na haya tunayoyaona.  Fikra yetu ni kua Taqwa hupatikana kwa kuswali lakini Qur’an inasema kwamba ukishaswali basi Imani utaipata punde tu utakapokuwa na Taqwa. Sisi hudhania kuwa mwanadamu hutoa sadaka ili awe na Taqwa, ila Quran inaeleza kinyume chake ya kwamba uwe na Taqwa kwanza kisha utoe sadaka.

 Tulikuwa tunachambua sura moja inayohusiana na nchi yetu ambayo ni ukosefu wa Taqwa katika mfumo wa kisiasa.  Dalili ya uwepo wa siasa bila Taqwa ni watu kujihusisha na wanasiasa wasio na huruma.  Wanasiasa hao ambao hawana uwezo wala vipaji vya kufanya siasa bali wanakuwa watawala wa jamii isiyokuwa na Taqwa.  Sifa mbaya zaidi ambayo imewasilishwa katika riwaya na Ahlulbayt (a) ni Hubbur Riyasah, ambayo ni tamaa, uchu na shauku ya uongozi na madaraka.  Mwanadamu anapoendeleza balaa hii ya kutaka kwa kila namna kuwa kiongozi wa umma, dini, siasa, mara nyingi huwa ni dalili tosha ya taifa na mtawala waliokosa Taqwa.  Wakati Fisk na Fujoor ambayo yenyewe ni aina ya ufisadi inapofikia kilele, ufisadi hugeuka kuwa saratani ambayo haipati matibabu kwa miaka na kutoa maumivu, usaha, damu kwa mwanadamu.  Ikiwa Taqwa itaharibiwa katika jamii na Fisk na Fujoor wanakuwa jamii yenye saratani ulioathiriwa na ufisadi huu wa nafsi, kisha tamaa hugeuka kuwa Hubbur Riyasah.  Kizazi cha sasa kimejiingiza sana katika janga hili, haswa katika nchi yetu. Adhabu kubwa kwa jamii hii ni wale watu ambao wana ugonjwa huu wa kupenda madaraka na umegeuka kuwa saratani ambayo inamsumbua kila mtu.  Kutokana na hili makundi yote ya maisha yanakabiliwa na matatizo.  Uchumi unaharibika kutokana na watu hawa wenye uchu wa madaraka ya kuwa viongozi wa nchi.  Kila sehemu ya nchi ni mwathirika wa uharibifu haswaa wa kiuchumi.  Mfumuko wa bei na kila hitaji muhimu la maisha limeenda nje ya uwezo wa mwananchi wa kawaida.  Tunahitaji kutafuta sababu ya jambo hili, vyombo vya habari na wanasiasa waliopo wamezama katika upotofu tu, hawatoi ukweli wa jambo lolote.

 Ahlulbayt (a) wameeleza kuwa ugonjwa huu unaweza kuharibu uchumi na kila kitu cha jamii pale inapotawaliwa na watu wenye uchu wa madaraka.  Dunia na Akhera zote zinaharibiwa.  Imamu Raza (a) na Imamu Sadiq (a) na katika vitabu vya Hadithi za Ahlu Sunna hali hiyo hiyo imesimuliwa na Mtume (a).  Ahlulbayt (a) pia wameisimulia hadithi hii ya mtume na kwa mujibu wa Hadithi hii mtu huyu ambaye ni mwabudu madaraka ni hatari zaidi kuliko mbwa mwitu wakali, wenye njaa wanaoshambulia kundi la kondoo lisilokuwa na mchungaji.  Uharibifu unaosababishwa na mbwa mwitu hawa juu ya kondoo ni mdogo kuliko viongozi ambao wana uchu wa madaraka.  Popote ambapo mwanadamu anakuza tamaa hii ya kuabudiwa na watu kwa kuwa kiongozi na hii ndiyo balaa ambayo Pakistan imezingirwa nayo kwa sasa.

 Kuna hadithi nyingi katika Kitabu hiki Mizan Al Hikmah, juzuu ya 4.

 Imam Ali (a) anasema kwamba Aafatul Ulamaa Hubbur Riyasat.  Msiba kwa Maulamaa ni kupenda uongozi.  Ni kwa ajili ya wote lakini kwa wanachuoni hili likiendelezwa linawaangamiza kabisa.  Kuna misiba mingi kwa wanachuoni iliyotajwa katika Hadith kutoka kwa Mtume na Ahlulbayt (a) waliopo katika Usuul al Kafi.  Wanachuoni wengi wa Sunni na Shia wameandika vitabu pia juu ya swala hili.  Imamu Gazali ameikusanya sura hii kwa uzuri sana na wanachuoni wengine wamechukua kutoka hapo.  Allama Majlisi katika Bihar ul Anwar ameanzisha kitabu kutoka katika sura hii.  Anawasilisha hadhi, kiwango cha Wanachuoni kwamba nafasi yao iko karibu na Mtume lakini wale wanachuoni ambao wana dalili za kiungu za kuwa mwanachuoni wapo, kwao kuna balaa moja la kawaida ambalo ni hili.  Mwanachuoni anapoingiwa na maradhi ya kiroho husitawisha upendo wa uongozi na hufuata kujipatia mamlaka.  Hadithi kutoka kwa Imam Sajjad (a) ambayo ni nzuri sana na inapaswa kukaririwa na muumini.  Mila hiyo ndiyo kigezo cha kivitendo cha dini na udini.  Katika mila hiyo magonjwa mengi yapo lakini yenye uharibifu zaidi ambayo yanaangamiza sio Alim tu bali Alam (ulimwengu).  Wakati Alim anapoharibika basi Alam, yaani ulimwengu unaangamizwa.  Makundi mawili yanapoharibika basi jamii nzima inakuwa fisadi, moja ni Alim pili ni Hakim.  Ufisadi wao unakuwa utamaduni na kutekelezwa katika jamii na watu pia wanapata mateso kwa kuwafuata.

 Nchini kwetu wanasiasa wanategana wao kwa wao, lakini ufisadi huu utaona upo katika makundi yote ya watu katika jamii.  Kitu kinapokuwa ugonjwa wa kijamii kinakuwa cha jumla.  Huu ni uwanja wa dini ambao ni kanuni za kijamii ambazo tumepuuza kutokana na kuzingatia kuwa ibada za kitamaduni  ndio dini pekee.  Bali dini hushamili muda wote wa maisha.  Sio kama inavyoitikadiwa  kwamba kuna muda wa mapumziko ambao uko nje ya dini.  Dini si kama duka au ofisi ambapo unaweza kupata muda wa kutoka nje ya mazingira ya kidini.  Kwani kila sehemu hata za kibiashara au ofisini, dini inayo mwongozo wa ajira ni kama tu kuwa msikitini.  Msikitini tunahisi tuko katika dini na hali hiyo hiyo inapaswa kuwa katika kila hatua ya maisha yetu.  Ofisini, mtaani, njiani, dukani, elimu, siasa kila mahali tunapaswa kuwa kama tuko msikitini tukitekeleza wajibu wa dini.

 Wakati magonjwa ya kijamii yanapokuzwa basi ugonjwa mkubwa zaidi ni ule unaokuza hamu ya uongozi ndani ya mwanadamu haswa kwa kundi la wanachuoni na watawala. Ugonjwa huu unapoathiri makundi haya mawili ni uharibifu wa taifa zima.  Iwapo mwanachuoni atapatwa na ugonjwa huu basi watu wanaomfuata nao watapatwa na ugonjwa huu.  Mfano ikiwa umekaa ndani ya basi huku unafanya Zikr ya Mwenyezi Mungu na wala  haujafanya dhambi yoyote maishani, lakini dereva wa basi ile awe amelewa basi katika hali hii pia utaangamia kwa sababu aliyeshika usukani amelewa.  Mfano huu pia umetoka kwa Imamu Sadiq (a) ambaye ametoa mfano wa mashua.  Anasema ikiwa ndani ya mashua ambapo watu wema na wabaya wote wameketi, na ikiwa mtu mmoja atatoboa shimo kwenye mashua hiyo basi kila mtu ataangamia.  Jamii pia ina hadhi ya mashua ambapo kila mtu anaharibiwa.  Alim na Hakim wote ni madereva wa basi, mmoja ana usukani wa dini na mwingine wa taifa.  Wote wawili wakilewa basi jamii itaangamia.  Leo, kwa mfano watu hawapati Samli ambayo ni zao la ndani ya nchi, kwa nini?  Hii ni kwa sababu aliyeshika usukani amelewa.  Amelewa na tamaa ya madaraka.  Serikali iliyopita ilivunja rekodi ya kuwa na uchu wa madaraka.  Katika historia nzima ya Pakistan uchu wa madaraka wa aina hiyo haikuwahi kushuhudiwa kwa mtu yeyote hapo awali nchini Pakistani.  Serikali ya sasa nayo ina uchu wa madaraka kwa ukali.  Wanatangaza kuwa tunatengeneza nyakati ngumu na kuliangamiza taifa, ni mtu  ambaye ni mlevi tu anayeweza kuzungumza hivi.  Mtawala akishalewa basi inabidi watu wateseke.  Hii ndiyo safari ya maangamizo ya watu ambao tumewapa uongozi.  Mfumo mzima uko hivi.  Na juu ya hii tumeongeza na demokrasia ambayo inaruhusu kila fisadi kuingia madarakani.  Uwezo huu unaotolewa na demokrasia unawezesha mfisadi kuwa mkuu wa watu waadilifu hivyo hivyo kwa kuwahadaa watu.

 Mtu wa pili ni mwanachuoni ambaye ana utawala juu ya mambo yote ya watu.  Iwapo mwanachuoni atakuwa mwanachuoni bila kujali ana elimu au la.  Yeyote ambaye watu wanamchukulia kama mwanachuoni wanamgeuza kuwa mwanachuoni na anachukua nafasi ya mwanachuoni.  Bila kujali kuwa msomi wa kweli au aliyepachikwa na mwanadamu ikiwa wataendeleza Hubbur Riyasah basi wao ndio watu wafisadi zaidi ambao wataharibu zaidi, hata zaidi ya hakim.  Leo udini, ugaidi na mabishano yameenezwa na wanazuoni.  Kuna wanachuoni walioundwa na mwanadamu na wengine ni wenye elimu ingawa hawana Taqwa.  Ikiwa Alim hana Taqwa basi anapelekea kwenye maangamizo.  Unaweza kuona mitandao ya kijamii iliyojaa wanazuoni wa aina hiyo wanaovunja umma wa Mtume, wakizusha mifarakano, wakiwasilisha Ghuluw ili kuligawa taifa.  Unaweza kuona uchafu wa wasomi hawa kwenye mitandao ya kijamii.  Ni wale wenye tamaa ya madaraka na uongozi. Ni Jinsi ambayo Mtume alivyotabiri kwamba wakati utakuja juu ya umma wangu ambapo Maruf itakuwa Munkar na Munkar itakuwa Maruf, ambapo watu watapenda Munkar.  Masahaba wakauliza “je wakati huu utafika kweli.”  Mtume (s.a.w.w.) alisema kibaya zaidi kuliko wakati huo kitakuja.  Wakati utakuja ambapo mwelekeo wa watu kuelekea Maruf utaisha na watakua wapenda maovu.  Mtu mbaya zaidi kati yao ni yule ambaye anakuwa kiongozi wao.  Unaweza kutazama jamii yako na makini na humo utakuta watu wa namna hii ambao wanachukiwa na dini, Mtume na Ahlulbayt (a) wanapendwa na jamii yetu.  Kila dhehebu limekusanyika karibu na utu fulani na jumuiya nzima imegawanyika.  Jaribu kutafuta na kuona kama kote Pakistani kuna watu ambao wamekusanyika karibu na Quran, Hablullah.  Unaweza kufanya uchunguzi wa sampuli na ujitambue.  Watu wamegawanyika na kukusanyika zaidi karibu na wale ambao wana tamaa na upendo wa mamlaka.  Wakati Ahlulbayt (a) wanasema yeye ndiye fisadi zaidi na ataharibu kila kitu chako.  Unaweza kuona huko Pakistan kwamba kila kitu kitaharibiwa.  Matibabu ni nini?

 Huwezi kumaliza tamaa yao ya madaraka.  Wanaweza kufa lakini hawataacha tamaa ya uongozi.  Hata ukiwatoa madarakani hawatashuka.  Kwa kila kiongozi uongozi ni kama ngozi.  Suluhu si kwamba wanaonywa na kuhubiriwa ili wawe watu wenye utu  na si viongozi tu.  Wanawezaje kuwa watu wa kawaida  baada ya juhudi kubwa walizozifanya ili kuwa viongozi?  

Watu wanaongozwa na riwaya hizi kwamba watu wanapaswa kujikinga na watu wenye ugonjwa kama huo na sio kupanda meli zao.  Tamaa ya mamlaka ina madhara mabaya zaidi ya Madawa ya kulevya hata kuliko cocaine na heroin ambayo madhara yake ni  ya muda mfupi lakini tamaa ya mamlaka huharibu taifa zima.

Katika riwaya inayofuata kutoka kwa HP

 Yeyote anayetaka watu wakusanyike kumzunguka, wamfuate, na wamkusanyie umati wa watu, mahali pake pa kupumzika ni moto.  Hii ina maana ya mtu anayetaka kuwa kiongozi ambaye sifa zake zimetajwa katika riwaya hii.

 Hadithi inayofuata kutoka kwa Imamu Sadiq (a)

 Anayetamani jina lake litajwe zaidi, awe mwenye kusifiwa kila mahali na kauli mbiu zake zikiinuliwa basi na atambue kuwa tabia hizi za kujidhihirisha haziji kwa mtu anayemcha Mungu.

 Tunaweza kupata sifa hizi kwa watu wengi na bado tukawafanya watu hawa kuwa wahenga na viongozi wetu wa kiroho.

 Imepokewa katika hadithi kwamba iwapo mwanachuoni fulani atakuwepo katika mkusanyiko na watu wanamheshimu, na akija mwanachuoni mwengine naye pia anaheshimiwa na watu, na kama mwanachuoni wa kwanza akiwa na hisia  kwamba yule wa pili hakupaswa kuheshimiwa.  basi moyo wa mtu huyu hauna upendo na hofu ya Mungu.

 Kuna Hadith ambayo Imam (a) anataja maradhi kumi ya wanachuoni.  Moja wapo ni husuda, ambayo kwa mujibu wa mapokeo mengine ni kwamba kati ya 10 za husda, sehemu 9 ni mahususi kwa wanachuoni na sehemu moja ni ya kila mtu.  Na katika sehemu hii moja iliyotengwa kwa wote, wanachuoni pia wana sehemu.  Unaweza kuona kuwa ugonjwa huu ni hatari sana kwani husuda iliyopo kwa mwanachuoni inaharibu dini na jamii.  Katika riwaya hiyo hiyo Hubbur Riyasah pia inatajwa kuwa ni ugonjwa mkubwa.  Mwenyezi Mungu ampe kila mmoja wetu wokovu kutokana na ugonjwa huu.

 

Hotuba ya 2:  Usizungumzie mambo ambayo Mwenyezi Mungu hakuyazungumzia.

Ramani ya Taqwa yenye maana ya Taqwa ya vitendo kwa misingi ambayo inaweza kutekelezwa katika maisha yetu.

Katika hekima ya 105, AM inawasilisha sera inayohusiana na Taqwa

 .  وَ قَالَ عليه السلام: إِنَّ اللَّهَ افْتَرَضَ عَلَيْكُمْ فَرَائِضَ فَلَا تُضَيِّعُوهَا وَ حَدَّ لَكُمْ حُدُوداً فَلَا تَعْتَدُوهَا وَ نَهَاكُمْ عَنْ أَشْيَاءَ فَلَا تَنْتَهِكُوهَا وَ سَكَتَ لَكُمْ عَنْ أَشْيَاءَ وَ لَمْ يَدَعْهَا نِسْيَاناً فَلَا تَتَكَلَّفُوهَا

 Amirul-mu’minin, amani iwe juu yake, amesema: Mwenyezi Mungu ameweka juu yenu baadhi ya faradhi ambazo hampaswi kuzipuuza, na amekuwekeeni mipaka ambayo msiikiuke na amekukatazeni baadhi ya mambo ambayo msiyakiuke.  Amenyamaza juu ya mambo fulani lakini hakuyaacha kwa kusahau, basi usijitwike nayo.

 Ikiwa tunasadiki anachosema Amirul Mumin (a) kwamba Mwenyezi Mungu ananyamaza juu ya baadhi ya mambo na wala hakuyagusia ndani ya Quran pia, basi tusijitie kwenye taabu. Kwani  chochote kilichokuwa muhimu kwa ajili ya uwongofu kilikuja ndani ya Qur’an na kisichokuja katika Qur’an si lazima kwa uwongofu.  Ukiona kuna baadhi ya mambo ambayo hayajaelezewa kwa uwazi kabisa ndani ya Qur’an lakini katika vitabu vya Tafsiri tunaona majadiliano mapana  juu ya haya.  Kwa mfano: Quran haikutaja ni mti gani ambao Adam aliukaribia.  Lakini katika vitabu vya Tafsiri kuna mjadala mwingi kuhusu mti huo.  Lau hili lilikuwa muhimu basi Mwenyezi Mungu angeupa mti huo jina, na kwakuwa hakulitaja basi ni kwa nini tunajipa dhiki kubwa! 

Tarehe za kuzaliwa kwa Mtume (saww) haikutajwa katika Quran,kwa kuwa haina uhusiano wowote na mwongozo.  Kwa hivyo kwa nini utumie muda mwingi hapo?  Vile vile Quran haijataja majina ya mke, au binamu wa Mtume Musa au idadi ya watu wa pangoni pamoja na kuwa  Qur’ani iliwalaani wale wanaobishana kuwa walikuwa wangapi.  Lau kungelikuwa na mwongozo katika idadi hizi basi zingelitajwa.

  Wakati Mwenyezi Mungu hajagusia baadhi  kwenye kitabu, Amirul Momineen (a) anasema haimaanishi ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwasahau.  Bali ni kwa kuwa kutajwa kwao hauna umuhimu kwa mwongozo.  Unaposoma Quran unaona baadhi ya maandishi yameandikwa chini kwenye Quran ili kukamilisha aya.  Jambo ambalo Mwenyezi Mungu hajalitaja basi wewe usiingie katika urasmi na ugumu wa kuthibitisha hilo.

 Katika Surah Maida, Mwenyezi Mungu ameongoza hili;  Mwenyezi Mungu anasema msiulize mambo mengi kwani yatakugharimu.  Shahid Husein (r.a) aliulizwa katika mkusanyiko kuwa ni nani aliyevaa kilemba cha kwanza katika historia.  Mtu huyu alitilia shaka uongozi wa Shaheed.  Mtu mmoja wa kawaida alisimama na kusema naweza kujibu.  Akasema, Nabii Nuhu ndiye wa kwanza aliyevaa.  Baadae Shaheed alipomuuliza umepata wapi? alisema  sijui pia ila nimefanya hivyo ili niondoe  shaka yake juu ya ujuzi wako.  Shaheed kisha akamkemea asifanye hivyo.

 Katika Surah Maida aya ya 101

 Kwa upande mmoja tumehamasishwa kuuliza maswali kuhusu yale mambo ambayo hatujui.  Kama vile unapaswa kufahamu juu ya majukumu yako, ambayo unapaswa kusoma na kuhoji pia.  Kisha tuulize kuhusu mipaka ya Mwenyezi Mungu, na vile vile tupate uvumbuzi juu ya mambo ya haramu.  Lakini kuna mambo fulani ambayo hatupaswi kuuliza, kwa sababu pindi tukiuliza hatutapenda majibu yake.

 Ndipo Aya inasema ukisisitiza juu ya kujua mambo fulani, pindi yakidhihirika basi utafadhaika.

 Katika mkusanyiko mmoja, mtu mmoja aliuliza juu ya ada ambayo kwa ujumla watu hufanya.  Nilisema sitajibu chochote kuhusu ada  hio.  Na pindi aliposisitiza  nikamwambia hautapenda jibu lake.  Quran inasema sawa kwamba msiulize mambo fulani, basi yafiche msiyo yapenda.  Wakati Mwenyezi Mungu hajafichua mambo fulani, basi kwa nini mnataka kuondosha sitara hizo!

Aya inasema kama ukiuliza kuhusu baadhi ya mambo wakati wa kuteremshwa Quran, basi huenda ikafichuka na utajuta.

 Katika msemo huu wa 105, Amirul-Muminin (a) anasema kwamba Mwenyezi Mungu alipitisha ukimya kwa baadhi ya mambo si kwa kughafilika au kusahau hivyo unapaswa pia kukaa kimya.  Hii ilikuwa ni kwa sababu hakuna mwongozo unaopatikana katika mambo hayo.  Amirul Momineen (a)  anasema ifanye Quran kuwa Imamu wako na usiwe Imamu wa Quran.  Ukifika mahali ambapo Quran inakwenda ifuate na pale Quran inaposimama unatakiwa usimame na usitangulie  Quran.  Vile vile kwa Uimamu.  Katika Swala tumefunzwa kufuata kila kipengele cha Swala, ambapo tunapaswa kumfuata Imamu wa Swala.  Ukimtangulia Imam wa Swala katika kipengele chochote kama vile kusujudu hata kwa sekunde moja basi hutafuati bali unaongoza Swala.  Tunapaswa kufuata Quran na Imam.

 Mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyanyamazia, nanyi pia nyamazeni, msihoji wala msitafiti.  Kwa aina fulani ya mwanachuoni imesemwa katika riwaya kwamba mwanachuoni huyu hajui chochote ambacho Mwenyezi Mungu amekiteremsha lakini kisichoteremshwa anajua kila kitu kuhusu hili.  Mujtahid mmoja alikwenda kwa Faqih kukutana naye alikuwa akifanya utafiti.  Akamwambia Faqih kwa nini unafanya mambo hayo kama faradhi, majukumu ambayo hayakutajwa na Mwenyezi Mungu.  IKIWA tutaishia katika kanuni hizi nne;  msiache wajibu, msivunje mipaka, mkataze maovu na mkanyamaze juu ya yale ambayo hayakutajwa na Mwenyezi Mungu, basi kuna uwongofu na Taqwa katika hili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *