Katika kutafuta mafanikio katika medani ya soka, timu ya Palestina imejitahidi kuleta matumaini na tabasamu kwa watu ambao ni waathiriwa wa vita.
Uwanja wa Kombe la Dunia la Seoul ni mojawapo ya medani za kandanda zinazohusisha watu wengi zaidi na zinazotisha. Ibada isiyoyumba ya mashabiki wa Korea Kusini – inayopakana na tamaa – inaweza kufanya timu kubwa kujisikia vibaya kwenye bakuli hili.
Siku ya Alhamisi, ingawa, mashabiki wa nyumbani walionyesha kwa ufahari bendera, skafu na mabango yenye kuunga mkono wapinzani wa Korea Kusini – Palestina.
Huku kukiwa na mashati mekundu, yanayoangazia rangi ya jezi ya timu ya nyumbani, sehemu kubwa ya uwanja huo wenye uwezo wa kumiliki kiwango cha watu 66,000 walienua bendera na kuonyesha ujumbe wa kuunga mkono kwa timu ya ugenini ambayo ni Palestina.
Hali ya kuhuzunisha ilitanda kwenye mazingira ya mechi ya kwanza ya Palestina katika raundi ya tatu ya mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Ulikuwa ni usiku wenye kukumbuku pale ambapo kikosi cha kocha Makram Daboub kilipoondoka uwanjana na pointi stahili na ya thamani kubwa baada ya sare ya sufuri dhidi ya wababe hao wa soka barani Asia, kutokana na juhudi na ufanisi wa kipa Rami Hamadeh na ukosefu wa weledi kutoka kwenye timu ya ya Korea Kusini.
Kupeperusha bendera kwa ajili ya Palestina
Wakati timu hiyo ikikabiliana na changamoto zake kuelekea 2026, Wapalestina huko Gaza wanaendelea kulengwa na wanajeshi wa Israel, ambao wameua zaidi ya watu 40,000 na kujeruhi zaidi ya 94,000, kulingana na Wizara ya Afya huko Gaza. Nchini Israel, watu 1,139 waliuawa katika mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyoongozwa na Hamas, ambayo yalianza vita vya sasa.