Hukumu ya Saudia Arabia dhidi ya daktari Mtunisia yapingwa na kulaaniwa vikali

Taasisi ya Kitaifa ya Kuunga Mkono Muqawama na Kupinga Kuanzishwa Uhusiano wa Kawaida na utawala haramu wa Israel ya nchini Tunisia imelaani vikali hukumu ya Saudi Arabia ya kumfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Taasisi hiyo ya kitaifa mbali na kulaani hukumu hiyo imeitaka Saudia imemuachilie huru mara moja daktari huyo wa kike raia wa Tunisia na kumuomba radhi.

Katika sehemu nyingine ya taarifa yake, Taasisi ya Kitaifa ya Kuunga Mkono Muqawama na Kupinga Kuanzishwa Uhusiano wa Kawaida na utawala haramu wa Israel ya nchini Tunisia imesisitiza himaya na uungaji mkono wake kwa Hizbullah ya Lebanon na kueleza kwamba, harakati za Hhizbullah ni mapambano ya kitaifa na wenzo wa mashinikizo ya kuhitimisha uvamizi wa Israel.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni mahakama moja nchini Saudi Arabia ilimuhukumu kifungo cha miaka 15 jela Bi Mahdiyah al-Barzouqi kwa madai ya kuuvunjia heshima utawala wa kiukoo wa Saudi Arabia.

Kosa pekee lililofanywa na daktari huyo raia wa Tunisia ni kuweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, video ya maandamano ya wananchi wa Tunisia waliokuwa wanaunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Televisheni ya al Mayadeen imemnukuu kaka wa daktari huyo akisema kuwa, dada yake mwenye umri wa miaka 51, amekuwa akiishi nchini Saudia tangu mwaka 2008 kwa ajili ya kufanya kazi ya udaktari.

Askari usalama wa ukoo wa Aal Saud walimkamata mwaka 2020 kwa kuweka kwenye ukurasa wake wa Twitter, maandamano ya wananchi wa Tunisia ya kuiunga mkono Hizbullah ya Lebanon.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *