Ibrahim Raeisi: Hakuna mazungumzo yoyote yatakayoifanya Iran ilegeze msimamo katika haki zake

Rais Ibrahim Raeisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakuna kikao au mazungumzo yoyote yale ambayo yatalifanya taifa hili lilegeze kamba na kufumbia macho haki zake.

Rais wa Iran amesema hayo leo katika mkutano wa 17 wa Siku ya Kimataifa ya Msikiti na kueleza kwamba, serikali inafanya kila iwezalo na kwa nguvu zake zote kuhakikisha kwamba, ustawi na maendeleo ya nchi yanapatikana sambamba na kuyatatua matizo yaliyopo.

Sayyid Ibrahim Raeisi amesisitiza kuwa, licha ya kuweko vikwazo na vitisho dhidi ya taifa hili, lakini serikali yake inaendelea kufanya kazi zake na kutekeleza mipango yake bila wasiwasi.

Rais wa serikali ya awamu ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesisitiza kuwa, hakuna kikao au mazungumzo yoyote yale ambayo yatalifanya taifa hili lilegeze kamba na kufumbia macho haki zake.

Ayatullah Raeisi ameashiria mikakati na mipango iliyotekelezwa na seriikali yake katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika uga wa kupambana na virusi vya Corona, kustawisha siasa za ujirani mwema, kuleta uwiano kkatika sera za kigeni, kuongeza biashara za nje sambamba na kufanya juhudi za kujitosheleza katika sekta mbalimbali.

Aidha amesema kuwa, taifa la Iran lina nguvu zenye mfungamano na wananchi na juhudi za serikali ya wananchi zimesimama juu ya msingi wa nguvu hii na inafanya hima kudhamini maslahi ya taifa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *