Idadi ya Makombora zaidi ya 20 yarushwa kuelekea vituo viwili haramu vya Marekani mashariki mwa nchi ya Syria

Mwandishi wa idhaa ya “Al-Alam” nchini Syria aliripoti kuwa zaidi ya makombora 20 yalirushwa katika vituo 2 haramu vya Wamarekani huko Deir Ezzor iliyoko kaskazini mashariki mwa Syria.

Siku ya Ijumaa usiku, zaidi ya makombora 20 yalirushwa katika vituo viwili haramu vya Marekani katika maeneo mawili ya mafuta “Al-Omar” na gesi “Konico” huko Deir Ezzor (mashariki mwa Euphrates), iliyoko kaskazini mashariki mwa Syria.

Ripota wa Al-Alam pia aliripoti kuruka kwa helikopta za Kimarekani kwenye uwanja wa gesi wa Koniko kufuatia mashambulizi haya ya roketi.

Kwa upande mwingine, afisa mmoja wa jeshi la Marekani ameuambia mtandao wa Al Jazeera wa Qatar kwamba moja ya kambi za Marekani mashariki mwa Syria ilipigwa na makombora 8.

Yeye, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisisitiza kuwa Washington inatathmini uharibifu wa shambulio hili la roketi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *