Idadi ya watu walioaga dunia katika machafuko yanayoendelea nchini Bangladesh iimeongezeka na kufikia watu 115.
Ripoti zaidii kutoka nchini humo zinasema kuuwa, jumla ya watu 115 wameuwawa nchini Bangladesh huku polisi wakipambana bila ukomo dhidi ya maandamano yanayoongozwa na wanafunzi kupinga nafasi za kazi za serikali licha ya marufuku iliyowekwa na mamlaka husika ya kushiriki katika mikusanyiko.
Mapema jana Ijumaa, mawasiliano ya simu pia yakatwa na vyombo vya habari kama radio na televisheni kutokuuwa hewani. Lakini pia mamlaka husika nchini Bangladesh zilikata baadhi ya huduma za simu za mkononi siku iliyopita ili kujaribu kuzima machafuko.
Pamoja na hatua hizo, siku hiyo hiyo wanafunzi waandamanaj walivamia gereza moja na kuwaachilia mamia ya wafungwa wakati polisi wakijitahidi kutuliza machafuko, na mikutano mikubwa.
Polisi waliweka amri kali ya kutotoka nje kwa amri ya “kupigwa risasi atakayeonekana wakati wa marufuku hiyo ya kutotoka nje” kote Bangladesh wakati vikosi vya jeshi vikishika doria katika maeneo ya mji mkuu Jumamosi baada ya watu wengi kuuawa na mamia kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokana na ugawaji wa kazi za utumishi wa umma.
Ijumaa ya jana ilielekea kuwa siku mbaya zaidi kufikia sasa; Somoy TV iliripoti kuwa watu 43 waliuawa, wakati mwandishi wa Associated Press aliona miili 23 katika Chuo cha Matibabu cha Dhaka na Hospitali, lakini haikujulikana mara moja ikiwa wote walikufa siku ya Ijumaa. Siku ya Alhamisi, watu wengine 22 waliripotiwa kufariki huku wanafunzi waliokuwa wakiandamana wakijaribu “kufunga kabisa” nchi.