Idadi ya waliokufa katika mlipuko wa lori la mafuta Nigeria yafikia 150

Idadi ya watu waliopoteza maisha baada ya lori la mafuta kuripuka na kusababisha moto mkubwa kaskazini magharibi mwa Nigeria imeongezeka na kufikia watu 150.

Kwa muji wa msemaji wa jeshi la polisi, Lawan Adamu lori hilo liliripuka kando ya barabara kuu ya Kano-Hadejia kwenye eneo la Taura la jimbo la Jigawa la kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Maafisa wa serikali za mitaa kaskazini mwa Nigeria jana waliungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya maziko ya umati ya zaidi ya wahanga 140 waliopoteza maisha katika mlipuko mkubwa wa lori la mafuta usiku wa kuamkia jana.

Maafa hayo yalitokea katika mji wa Majiya katika jimbo la Jigawa kaskazini mwa Nigeria wakati lori la mafuta lililopinduka lilipowaka moto huku umati wa watu ukijaribu kukusanya mafuta yaliyokuwa yakivuja kutoka kwenye lori hilo. Mlipuko huo umesababisha uharibifu mkubwa huku aghalabu ya miili ya wahanga ikishindwa kutambuliwa.

Maafisa husika wa Nigeria wamewatembelea baadhi ya manusura wa ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Matukio kama hayo ni jambo la kawaida nchini Nigeria. Mwanzoni mwa mwezi uliopita wa Septemba, makumi ya watu walipoteza maisha baada ya lori la mafuta kuripuka kaskazini mwa Nigeria.

Limekuwa jambo la kawaida huko Nigeria ambapo watu wengi huhatarisha maisha yao kwa kukimbilia malori yanayopinduka ili kuchota mafuta hasa ukizingatia kupanda kwa bei ya mafuta nchini tangu serikali ilipositisha mpango wake wenye gharama kubwa wa kufadhili ruzuku ya gesi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *