Idadi ya wanaotaabika kwa njaa duniani yaongezeka kwa zaidi ya 50%

Idadi ya watu wanaotaabika kwa baa kali la njaa duniani imeongezeka kwa zaidi asilimia 50 huku miito mbalimbalii ikiendelea kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia wenye njaa ulimwenguni.

Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Save the Children limetangaza katika ripoti yakke mpya kwamba, idadi ya watu wanaoteseka kutokana na njaa sasa imefikia miilioni 25,300,000 baada ya kuongezeka kwa asilimia 57.

Ripoti hiiyo inaeleza kuwa, nchi ambazo zina idadi kubwa zaidi ya watu wanaokabiliwa na baa la njaa ni Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Haiti, Somalia, Sudan, Yemen na Sudan Kusini.

Sehemu nyingine ya ripoti hiyo ya Shirika la kimataifa la misaada ya kibinadamu la Save the hildren inabainisha kwamba, Afghanistan ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na ukosefu wa usalama wa chakula ambapo idadi ya wanaotaabika kwa njaa imefikia milioni 6.6 mwaka huu kutoka milioni 2.5 mwaka 2019.

Likitegemea ripoti ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), shirika la Save the Children linasema, kwa sasa ulimwengu unakabiliwa na hali mbaya zaidi ya baa la njaa na kwamba, takribani watoto milioni 60 walio chini ya umri wa miaka 5 yumkini mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu wakakumbwa na utapiamlo na lishe duni.

Hivi karibuni zaidi ya asasi 200 za kiraia zilitoa mwito wa kuchukuliwa hatua kwa ajiili ya kukabiliana na janga la njaa ulimwenguni ambalo linazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *