Ikulu ya Marekani: Hali nchini Iraq inatia wasiwasi

Ikikanusha taarifa za kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad, Ikulu ya White House iliitaja hali ya Iraq kuwa yenye kutia wasiwasi na kutoa wito wa kudumisha amani na kuwepo kwa mazungumzo.

Siku ya Jumatatu, Ikulu ya Marekani ilidai kuwa taarifa za kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Iraq si za kweli.Taarifa kuhusu kuhamishwa kwa ubalozi huo ni za uongo na kwamba Kuhakikisha usalama wa wafanyikazi wa serikali, raia wa Amerika na usalama wa vifaa vya Amerika ndio jambo lenye umuhimu zaidi .

Ikulu ya White House imesema katika taarifa yake: Sasa ni wakati wa mazungumzo, sio kuongezeka kwa migogoro. Tunatoa wito kwa mikondo yote ya kisiasa nchini Iraq kudumisha utulivu na kuepuka vurugu na kutatua migogoro ya kisiasa kupitia michakato ya kisiasa chini ya usimamizi wa Katiba ya Iraq.

Taarifa hiyo imesema kuwa, ripoti za machafuko nchini Iraq, katika hali ambayo taasisi za Iraq haziruhusiwi kufanya kazi, zinatia wasiwasi. Hii huongeza hatari ya vurugu. Usalama, utulivu na uhuru wa Iraq haipaswi kuhatarishwa.

Kufuatia kauli ya Moqtada Sadr na tangazo la kujiondoa katika shughuli za kisiasa, idadi kadhaa ya waandamanaji wa harakati ya Sadr walimiminika mitaani na kuingia katika ikulu ya rais katika eneo la kijani kibichi la Baghdad katikati mwa mji huu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *