IMF:Iran nchi ya 21 yenye nguvu kiuchumi duniani

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umesema kuwa, Iran ni nchi ya 21 yenge nguvu kiuchumi duniani na kwamba nchi 171 duniani mwaka huu wa 2020 zimekuwa na uchumi wa kiwango cha chini ikilinganishwa na Iran.

Shirika la IMF limetabiri katika ripoti yake mpya juu ya kiwango cha uzalishaji wa ndani wa nchi 192 duniani ikiwemo Iran katika mwaka huu wa 2022. Taasisi hiyo ya kimataifa imeeleza kuwa, inataraji uzalishaji wa ndani nchini Iran kwa mujibu wa vigezo vya uwezo wa manunuzi mwaka huu wa 2022 utafikia thamani ya dola bilioni elfu moja na 599; kiwango ambacho ni ongezeko la dola bilioni 150 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Kwa kuwa na kipato cha dola elfu moja na 599 kutokana na uzalishaji wa ndani  Iran imetambuliwa  katika takwimu za shirika la IMF kuwa nchi ya 21 yenge nguvu ya kiuchumi duniani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uchumi wa Iran umezipita chumi za nchi nyingine 171 duniani na ni nchi 20 tu ambazo zitakuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa ndani kuliko Iran mwaka huu

Poland, Thailand, Pakistan, Uholanzi, Argentina, Afrika Kusini, Imarati, Uswisi, Ubelgiji, Sweden, Austria, Norway, Ureno, Finland na Belarusia ni kati ya nchi zilizo na uchumi mdogo mwaka huu kulinganisha na Iran.  Mfuko wa Fedha Duniani aidha umetangaza uchumi wa China kuwa uchumi mkubwa zaidi duniani kwa kuwa na uzalishaji wenye thamani ya dola elfu 30 na 74 katika mwaka huu wa 2022.

Aidha nchi ndogo yenye uchumi mdogo zaidi duniani kwa mujibu wa IMF ni wa nchi ndogo ya Tuvalu inayopatikana katikati ya Hawaii na Australia katika Bahari ya Pacific Kusini  ikiwa na uzalishaji wa ndani wa dola milioni 63 kwa mujibu wa vigezo vya uwezo wa manunuzi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *