Infantino: Nchi za Ulaya zinafanya unafiki, hazina hadhi ya kutoa somo la maadili

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino, amezishambulia nchi za Magharibi zinazoiandama Qatar, mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia, eti kwa rekodi yake ya haki za binadamu, akisema hatua inayochukuliwa na wakosoaji ni ya kinafiki.

Katika mkutano wake na waandishi habari mjini Doha, siku moja kabla ya kuanza mashindano ya Kombe la Dunia Qatar 2022 kesho Jumapili, Gianni amesema yanayosemwa na nchi za Magharibi kuhusu rekodi ya haki za binadamu nchini Qatar ni unafiki wa hali ya juu na kuongeza kuwa: Kila mtu anapaswa kuwa huru kumuunga mkono mtu au kundi lolote analolotaka.

Amesema nchi za Ulaya zinapaswa kuomba radhi kwa vitendo vyao katika historia. Amesema kwa kile ambacho nchi za Ulaya zimekifanya kwa miaka 3000 iliyopita ziapaswa kuomba msamaha kwa miaka mingine 3000 ijayo kabla ya kuanza kutoa somo la maadili kwa watu wa mataifa mengine.

Qatar imeharamisha mahusiano ya kingono baina ya watu wenye jinsia moja, na wataokutwa na hatia huenda wakafungwa hadi miaka mitatu jela. Vilevile imepiga marufuku matumizi ya pombe na vileo kwenye viwanja vya mpira wakati wa mashindano ya soka ya Kombe la Dunia yanayofungulia rasmi kesho kwa mechi baina ya mwenyeji Qatar na Ecuador.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *