Iran na Zimbabwe kusaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe zinanatazamiwa kusaini hati kadhaa za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ndani ya wiki kadhaa zijazo.

Hayo yamesemwa na Solat Mortazavi, Waziri wa Leba na Masuala ya Kijamii wa Iran katika mazungumzo yake hapa jijini Tehran jana Jumamosi na Dakta Sekai Nzenza, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zimbabwe.

Bila kutaja tarehe au siku maalumu, Waziri wa Leba na Masuala ya Kijamii wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Zimbabwe zitasaini hati kadhaa za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano karibuni.

Dakta Sekai Nzenza, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Zimbabwe yuko nchini kushiriki duru ya kwanza ya Kongamano la Kimataifa la Wanawake Wenye Ushawishi, lililomalizika jana.

Wiki iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Zimbabwe ziliazimia kupanua zaidi ushirikiano wao katikka nyanja mbalimbalii ukiwemo uga wa michezo.

Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha tisa cha Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na taifa la Kiafrika la Zimbabwe kilichofanyika hapa mjini Tehran Januari 16.

Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ya Kiafrika ambayo kwa miaka mingi sasa imekuwa na uhusiano mzuri na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *