Iran: Utawala haramu wa Israel siku zote umekuwa tishio dhidi ya amani na usalama wa kimataifa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, misingi ya utawala wa kibaguzi wa Israel imejengeka juu ya uvamizi na tishio kwa amani na usalama wa dunia.

Akiashiria mauaji ya Sabra na Shatila yaliyofanywa na utawala dhalimu wa Israel huko Lebanon katika kambi za wakimbizi wa Kipalestina mwaka 1982, Nasser Kan’ani Chafi ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwamba, leo tarehe 16 Septemba imepita miaka 40 tangu kutokea jinai za kutisha za siku tatu za mauaji ya umati dhidi ya wakimbizi wa Kipalestina katika kambi za Sabra na Shatila kusini mwa Beirut mji mku wa Lebanon yaliyofanywa na utawala unaomwaga damu wa Israel na washirika wake; hii haikuwa jinai ya kwanza na wala siyo ya mwisho ya utawala huo katili.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, misingi ya utawala wa ubaguzi wa rangi wa Israel imejengeka juu ya uvamizi, jinai na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Leo Ijumaa tarehe 16 Septemba ni kumbukumbu ya ukatili wa kinyama uliotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kambi za Wapalestina za Sabra na Shatila mjini Beirut Lebanon.

Katika tukio hilo la Septemba 16 mwaka 1982, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walishambulia kambi za wakimbizi wa Kipalestina za Sabra na Shatila mjini Beirut na kuwaua shahidi Wapalestina zaidi ya 3500.

Mauaji hayo ya umati yalitekelezwa kwa amri ya Ariel Sharon ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Israel. Mauaji hayo yalinyamaziwa kimya na vyombo vya habari; na hata madola yanayodai kutetea haki za binadamu ikiwemo Marekani na nchi za magharibi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *