Iran: Wazayuni hawaelewi lugha yoyote isipokuwa mabavu na vita

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni hauelewi lugha nyingine yoyote isipokuwa mabavu na vita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo leo Jumanne katika sherehe za kuenzi haki za binadamu na heshima ya mwanadamu hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, inasikitisha kuona kwamba katika dunia ya leo, nchi za Magharibi zinafanya njama za kuyatwisha mataifa mengine mambo yao chapwa tena katika hali ambayo nchi hizo za Magharibi zikiongozwa na Marekani haziko tayari kuheshimu hata masuala ya kimsingi kabisa ya haki za binadamu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, nchi ya Iraq ilikaliwa kwa mabavu na wanajeshi wa Marekani kuanzia 2003 hadi 2011. Karibu wanajeshi laki moja na 75,000 wa Marekani walitumwa nchini humo huku maeneo yenye utajiri wa mafuta ya nchi hiyo yakiwa ndani ya makucha ya kikoloni ya Uingereza.

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, Marekani na nchi za Magharibi ndio wadhamini wakuu wa silaha zinazotumiwa na magenge ya kigaidi, ili mbali na kuvinufaisha viwanda vya silaha vya Marekani na nchi nyingine za Magharibi, vitendo hivyo vya kigaidi vitumiwe pia kuhalalisha uwepo wa madola ya kibeberu katika eneo hili na kuutia nguvu utawala wa Kizayuni wa Israel.

Amesema, kwa kuzingatia yote hayo, hakuna kilichobakia kwa mataifa ya wanyonge na eneo la Asia Magharibi sipokuwa muqawama na kusimama kidete kupambana na jinai na njama zote hizo za Kizayuni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *