Ali Reza Akbari, jasusi wa shirika la kijasusi la Uingereza amenyongwa leo nchini Iran.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Mahakama ya Iran, Ali Reza Akbari, aliyekuwa na uraia pacha wa Iran na Uingereza, alipatikana na hatia ya kueneza ufisadi katika ardhi na kushiriki katika njama kubwa dhidi ya usalama wa ndani na wa nje wa Iran kwa kuifanyia ujasusi serikali ya Uingereza.
Baada ya kesi yake kusikkilizwa mahakamani, alipatikana na hatia na hukukumiwa kunyongwa na tayari hukumu hiyo ya kumnyonga jasusi huyo imeshatekelezwa.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, kwa miaka kadhaa, Akbari alichukua hatua zilizo dhidi ya usalama wa taifa la Iran na alifanya ujasusi kwa maslahi ya serikali ya Uingereza. Alikuwa na uhusiano na Shirika la Kijasusi la M16 la Uingereza na alifanya mikutano kadhaa na maafisa wa kijasusi wa adui katika nchi mbali mbali. Kwa muda mrefu aliendeleza ujasusi ambao ni uhaini dhidi ya usalama wa ndani na nje ya Iran ambapo shughuli zake hizo za ujasusi zilivuruga pakubwa nidhamu ya umma nchini Iran.