Israel imewafanyia ujasusi wafanyakazi wa asasi za kirai za Palestina

Shirika moja la kutetea haki za binadamu la Ulaya limefichua kuwa, programu ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni ya Pegasus imetumika kuwachunguza na kuwafuatilia wafanyakazi wa asasi za kiraia za Kipalestina, hususan zilizowekwa kwenye eti ya orodha ya ugaidi ya Tel Aviv.

Faraan: Shirika la Front Line Defenders lenye makao yake Ireland lilisema jana katika ripoti yake ya uchunguzi kuwa, vyombo sita vya mawasiliano vya wanaharakati wa haki za binadamu wa Palestina vimedukuliwa kwa kutumia programu hiyo ya Wazayuni.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, watu watatu kati ya sita waliolenga katika ujasusi huo wa Wazayuni, ni maafisa wa mashirika ya kibinadamu ya Palestina yaliyowekwa katika orodha ya ugaidi na utawala haramu wa Israel mwezi uliopita.

Jamii ya kimataifa imekosoa vikali kitendo cha Israel cha kuyaweka mashirika ya kiraia ya Kipalestina ya Addameer, al-Haq, Asasi ya Kuwalinda Watoto Wapalestina, Umoja wa Kamati za Wakulima, Kituo cha Utafiti na Maendeleo cha Bisan, na Muungano wa Kamati za Wanawake za Palestina, katika orodha yake ya makundi ya kigaidi.

Wazayuni wanavyodukua mawasiliano ya rununu kupitia programu ya Pegasus
Julai mwaka huu, uchunguzi uliofanywa na mashirika 17 ya habari yanayofanya kazi chini ya kundi lisilo la kiserikali la Forbidden Stories lenye makao makuu yake mjini Paris ulionyesha kuwa, programu hiyo iliyotengenezwa kwa kibali cha shirika la utawala haramu wa Israel la NSO, imefanikiwa au kufeli kudukua simu erevu za wanahabari, maafisa wa serikali na wanaharakati wa haki za binadamu wapatao 37 na kwa ujumla imeweza kutumika kulenga simu zisizopungua elfu 50 katika maeneo tofauti duniani.

Shirika la Kizayuni la NSO lilidai kuwa, programu hiyo imetengenezwa eti kwa ajili ya kupambana na ugaidi, madai ambayo hayana msingi wowote. Hii ni katika hali ambayo, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ni mmoja wa wahanga wa programu hiyo ya kijasusi ya Wazayuni ya Pegasus.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *