Je, Israel itaweza kuilinda Imarati dhidi ya ndege zisizo na rubani na makombora ya vikosi vya Yemen?

Wayemen wamesisitiza mara kwa mara kwamba vita vya muungano wa Saudia na Imarati dhidi ya Yemen katika kipindi cha miaka saba iliyopita kiuhakika ni vita vya Israel na Marekani, na kwamba tawala hizi mbili za Kiarabu na baadhi ya mamluki wengine wa kanda ya Kiarabu ni maonyesho tu ya vita hivi.

Sisitizo la ajabu la Saudi Arabia na Imarati la kuendeleza vita vya kipuuzi dhidi ya watu wa Yemen, ambavyo havijapata mafanikio yoyote isipokuwa uharibifu kwa eneo na mataifa yake, na pia kuondolewa kwa hazina za Saudia na UAE, hili linathibitisha ukweli kwamba sisitizo hili – kama vile vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vilitangaza pia – ni kwa amri ya viongozi wa tawala hizi za Riyadh na Abu Dhabi.

Hivi karibuni gazeti la lugha ya Kiebrania la Times of Israel liliwanukuu maafisa wa Israel wakisema kuwa, Tel Aviv inaishinikiza serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani iorodheshe harakati ya Ansarullah ya Yemen kuwa ni harakati ya kigaidi kutokana na ombi la Imarati.

Vyanzo vingine vya habari pia vimefichua kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu umeiomba serikali ya Biden kuitambua Ansarullah ya Yemen kuwa ni kundi la kigaidi na kulijumuisha jina lake katika orodha ya mashirika ya kigaidi.

Kwa mantiki hiyo, Baraza la Usalama la Taifa la White House linakusudia kuorodhesha Ansarullah ya Yemen  kama kundi la kigaidi katika orodha ya mashirika na makundi ya kigaidi, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikipinga kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wa harakati hiyo na kuliweka kundi zima katika orodha hiyo ya makundi ya kigaidi.

Jambo la kuzingatia katika suala hili ni shinikizo la Israeli kwa serikali ya Biden; Hii ni kwa kua utawala huo unahofia hatua ya Ansarullah na ushiriki wa Tel Aviv katika vita dhidi ya Yemen.Kama ambavyo vyanzo vilivyoeleza : “Wataalamu na wajuzi wengi wa nchi ya Israel wamesisitiza kwamba mashambulizi ya Ansarullah dhidi ya Imarati ni tishio la wazi kwa Israel, ambayo ina maana kwamba Israel pia iko katika kufikiwa na Wahouthi.

Hivi leo Imarati inauona utetezi wa Israel kuwa ndio hakikisho kubwa zaidi la kunusurika kutokana na mashambulizi ya Yemen; Kwa hivyo, anasisitiza juu ya kuendeleza vita dhidi ya Yemen. Lakini UAE bila shaka itazingatia upya hesabu zake za jana, kufuatia kupenya kwa ndege isiyo na rubani ya Hizbullah ya Lebanon (Hassan UAV) katika Palestina inayokaliwa kimabavu. Kiukweli, ni vipi serikali ambayo haijaweza kuizuia ndege isiyo na rubani ya “Hassan” itaweza kulitetea taifa la UAE ? !

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *