Katika kikao na Rais wa Iran Ayatullah Sayyed Ibrahim Raisi, Rais wa Russia amesisitiza kuwa: Uhusiano kati ya Moscow na Tehran ni wa kina na wa kistratijia, na nchi hizo mbili ziko katika mawasiliano ya mara kwa mara katika maingiliano ya kisiasa na masuala ya usalama, na nchini Syria wanaukaribu mkubwa wakikazi.”
Idhaa ya habari ya Kremlin iliripoti kua; Rais wa Russia Vladimir Putin alikutana kando na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ibrahim Raisi wakiwa katika mkutano wa ngazi za juu wa majimbo ya Caspian katika mji mkuu wa Turkmenistan usiku wa Jumatano.
Akimkaribisha Bw. Raisi, Putin alisema: “Uhusiano wetu kwa hakika una sura ya kistratijia ya kina, na kwa hakika tuna masuala mengi ya kujadili, na nimefurahishwa sana na fursa iliyojitokeza kuhusiana na suala hili.”
Aidha alikumbusha kua: Russia na Iran zinawasiliana mara kwa mara kuhusiana na masuala ya kisiasa na ya kiusalama. Mahusiano kati ya nchi hzi mbili ni ya kina na ya kistratijia. Tunawasiliana mara kwa mara katika mwingiliano wa kisiasa, kuhusu maswala ya usalama, tunafanya kazi kwa karibu katika maeneo muhimu kama kama vile Syria.
Rais wa Russia aliendelea kusema: “Ni mwaka jana tu, mauzo ya mabadilishano ya kifedha kati ya Russia na Iran yameongezeka kwa 81% na katika miezi ya kwanza ya mwaka huu kumekua na ongezeko la 31% nyingine, na hali hii ni ya kuridhisha na kwa maslahi ya nchi zote mbili. ”
Vilevile Rais Putin alimtakia heri Ayatullah Ali Khamenei, kiongozi Muadhamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Wakati wa mkutano na Vladimir Putin huko Ashgabat, Rais wa Iran Ebrahim Ra’isi alisema: “Russia na Iran zinaweza kufanya kazi kwa karibu sana katika nyanja ya usafiri, uvuvi na utalii katika bonde la Bahari ya Caspian.”
Raisi pia alibainisha kuwa mikataba yote ya awali kati ya nchi hizo mbili inatekelezwa na kufuatiliwa, na kwamba hayo ni maendeleo mazuri sana.
Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa 6 wa Caspian jana, Rais wa Russia alisisitiza kuwa Shirikisho la Urusi linapenda kuzidisha ushirikiano kati ya majimbo matano ya Caspian ya Russia, Azerbaijan, Iran, Kazakhstan na Turkmenistan, zikiwemo nyanja za kisiasa na zile za kiusalama. Aidha Putin alisisitiza kuwa kuzingatiwa kwa Mkataba wa Hali ya Kisheria ya Bahari ya Caspian ndio ufunguo wa ustawi wa eneo hilo.
Wakati wa mkutano na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Vladimir Putin alimshukuru kwa mawazo yake muhimu na ya kuvutia kwa maendeleo zaidi ya ushirikiano wa kimataifa katika eneo la Caspian.