Jebeli: Vikwazo dhidi ya IRIB ni mfano wa wazi wa udikteta dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB amesema kuwa vikwazo lilivyowekewa shirika hilo ni mfano wa wazi wa udikteta dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza na shirika la habari la Fars kuhusu udikteta wa vyombo vya habari vya Magharibi vinavyopinga mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, Peyman Jebeli ameongeza kuwa: kunashuhuiwa ukiukaji wa wazi kati ya nara na vitendo kwa wale wanaodai uhuru wa kusema na demokrasia na kuheshimiwa jamii; ambapo mfano wa wazi wa jambo hilo ni ukikaji wa haki za binadamu unaofanywa na Marekani kwa kuliwekea vikwazo Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB.

Jebeli ameeleza kuwa, IRIB ni shirika la utangazaji la taifa la nchi huru na kwamba shirika la IRIB huzalisha maudhui, kutangaza habari na kusaidia maendeleo ya nchi kulingana na mahitaji na hali ya jamii na nchi.

Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa pale taasisi za kiistikbari za Magharibi na kimataifa zinapoiwekea vikwazo IRIB zinadhihirisha namna unavyotokea kwa urahisi udikiteta na ukiukwaji huo wa madai ya uhuru wa kujieleza, ambayo yameziba masikio ya dunia nzima kwa miaka mingi.

Jebeli amehoji, ni vipi vyombo vya habari vya Magharibi usiku na mchana vinafanya kazi kwa uhuru kamili katika kitovu cha Ulaya kwa kuibua fitina, kutoa mafunzo ya kubua fujo na kupindua serikali na kuvuruga usalama wa Iran na wa nchi nyingine; bila kuchukuliwa hatua  yoyote ya kisheria? Lakini Shirika la Utangazaji la IRIB ambalo ni chombo cha habari mahususi cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na linalofanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni kwa maoni yao linakiuka sheria na hawawezi hata kustahimili kuwepo kwa shirika na chombo hiki kwenye satelaiti?

Umoja wa Ulaya tarehe 14 Novemba mwaka huu liliiwekea vikwazo televisheni inayorusha matangazo kwa lugha ya Kiingereza ya hapa nchini ya Press TV na shakhsia na taasisi kadhaa za Iran. Wakati huo huo shirika la Eutelsat la Ufaransa pia  limetangaza kuwa limesitisha shughuli zote za utangazaji za shirika la IRIB.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *