Jenerali wa Marekani: Iran haikulenga kutushambulia katika mji wa Erbil, makombora ya Iran yanauwezo wakufika Tel Aviv kwa urahisi

Jenerali mkuu wa Marekani amesema kuwa shambulizi la makombora la IRGC mjini Erbil halikuwa na nia ya kushambulia maeneo ya Marekani.

Kenneth McKenzie, kamanda wa shirika la kigaidi la Centcom, alisema siku ya Jumanne kwamba Iran haikua na nia ya kulenga nyadhifa za Marekani katika shambulizi la kombora huko mjini Erbil.

McCannie, ambaye alihudhuria mkutano wa Senaa Kuhusiana na shambulio la kombora la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwenye makao makuu ya Mossad mjini Erbil amesema: “Sio imani yetu kwamba shambulio la wikendi – yaani, shambulio la kombora – kwa kweli lilikuwa shambulio katika sehemu zetu. “Tunaamini kwamba shambulizi la kombora la Iran lililenga maeneo mengine.”

Katika sehemu nyingine ya madai yake, kamanda huyo wa shirika la kigaidi la Centcom amesema kuwa, wasi wasi wake mkubwa katika ngazi ya kijeshi na Iran ni kuhusiana na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo. Alisema: “Katika ngazi ya kijeshi, wasiwasi wangu katika nafasi ya kwanza ni kwamba hawamiliki silaha za nyuklia,”

Akaongeza kwa kusema: “Lakini pia nina wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko kubwa la idadi na ufanisi wa kikosi chao cha makombora ya balistiki, mpango wao wa ndege zisizo na rubani na makombora yao ya safari za ardhini,”

McKenzie alisema kuwa Iran kwa sasa ina makombora 3,000 ya balestiki, “ambayo baadhi yanaweza kufika Tel Aviv.”

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *