Jeshi la Uganda limetishia kumfukuza balozi wa Marekani nchini humo

Kufuatia vikwazo vya hivi karibuni vya Washington dhidi ya maafisa wanne wa polisi wa nchi hiyo, kamanda wa jeshi la Uganda alimuonya balozi wa Marekani kwamba anapaswa kuondoka katika nchi hio ya Afrika Mashariki ikiwa hatamuomba radhi rais wa Uganda.

Muhozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi ya Uganda, alimuonya Balozi wa Marekani nchini kwamba ikiwa hatamuomba radhi Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa kumtusi, atalazimika kuondoka nchini humo kufikia Jumatatu.
Kainrubaga ambaye ni mtoto wa rais wa Uganda, aliandika kwenye chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba William Pope, balozi wa Marekani nchini Uganda, alimdharau rais wa Uganda na kukiuka katiba ya nchi hiyo.
Aliendelea kusema kuwa balozi wa Marekani amemkosea heshima Museveni pekee, bali pia serikali na watu wa Uganda. Mkuu wa majeshi ya Uganda alisema: “Hili si suala la kibinafsi kati yangu na balozi wa sasa wa Marekani nchini Uganda, bali ni suala la kitaifa na utaona kwamba hakuna nchi ya kigeni itakayowahi kuitawala Uganda tena.”
Hakufafanua hatua za balozi wa Marekani, lakini tukio hilo limekuja baada ya Washington wiki iliyopita kuwawekea vikwazo maafisa wanne wa polisi wa Uganda kwa ukiukaji wa haki za binadamu.
Jumatano iliyopita, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, alitangaza kwamba maafisa wanne wa polisi wa Uganda watawekewa vikwazo kwa “kukiuka haki za binadamu na kufanya mateso na tabia ya udhalilishaji, unyama na ukatili”.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *