Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwauwa kwa makusudi raia wa Palestina

Jeshi la utawala wa Kizayuni limetoa taarifa na kukiri kwa namna isiyo rasmi kwamba lilimlenga na kumuua shahidi mwanamme wa Kipalestina bila ya sababu yoyote ile.

Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa, shahidi Ahmad Hassan Kahlah ambaye wiki iliyopita aliuliwa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo huko Silwad katika mji wa Ramallah hakuwa hatari yoyote kwa wanajeshi hao na aliuliwa makusudi na bila sababu yoyote.

Uchunguzi uliofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni unaonyesha kuwa, shahidi Kahlah ambaye alipigwa risasi shingoni na wanajeshi wa utawala huo na kufa shahidi hakuwa na lengo lolote la kufanya oparesheni ya kimuqawama au kuwashambulia wanajeshi wa Israel kwa silaha baridi kinyume na madai yaliyotolewa.

Hii ni katika hali ambayo, jeshi la utawala wa Kizayuni awali lilidai kuwa, raia huyo wa Palestina alikuwa amebeba silaha baridi na alikusudia kuwashambulia wanajeshi wa utawala wa Kizayuni na ndio maana walimpiga risasi.

Hii si mara ya kwanza kwa jeshi la utawala wa Kizayuni kukiri kuwauwa makusudi Wapalestina lakini pamoja na hayo hakuna wakati ambapo wanajeshi wa Israel wameshtakiwa na kuhukumiwa kwa jinai wanazozitenda dhidi ya raia wa Palestina.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *