Jeshi la Yemen limesema kuwa limerusha kombora katika chumba cha operesheni cha UAE katika mkoa wa Shabwa (kusini mwa Yemen).
Asubuhi ya leo (Jumanne) Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Sari, ametangaza kwamba kombora limerushwa kwenye Jumba la Operesheni la UAE na mamluki wake lililopo katika maene ya kusini mwa Yemen.
Msemaji huyo wa Jeshi la Yemen alisema yafuatayo: “Namshukuru Mwenyezi Mungu, kitengo cha makombora kiliweza kulenga chumba cha operesheni kilichopo katika uwanja wa adui, Imarati (UAE) wakishirikana na mamluki wake katika mji wa Asilan mkoani Shabwa kwa kombora la balestiki jana jioni siku ya Jumatatu “Tukio hili lisababisha viifo vya watu wengi wakiwemo raia wa Imarati huku baadhi yao wakijeruhiwa .”Yahya Sari aliongeza kuwa chumba hicho cha operesheni kilitumika kusimamia vita vilivyopo katika jimbo la Shabwa.
Kufikia sasa Jeshi la Yemen limetangaza mashambulio matatu ya makombora kwa kutumia ndege zisizo na rubani ndani ya Imarati.Mashambulizi ya jeshi la Yemen dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu yalianza tena baada ya Mohammed al-Bakhiti, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen, kuiambia Al-Arabi: “Kuna makubaliano kati ya Saudi Arabia na UAE, ya kwamba Saudi Arabia itakabidhi majimbo yote ya kusini mwa Yemen, pamoja na Shabwa, kwa UAE, na malipo yake ni kua, UAE itatumia uwezo wake wote wa kijeshi dhidi ya Yemeni kama ilivyokua zamani.”
Al-Bakhiti alionya kua: “Kuanzia sasa, tunaishauri Imarati kutoendeleza vitendo vyake vya kivita, kwa sababu ikiwa makabiliano hayo hayo yataendelea basi Yemen italazimika kushambulia maeneo ya ndani kabisa mwa ardhi yake. “Tupo tayari kivita.”