Mjumbe mwandamizi wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umesambaza kwa makusudi virusi vya corona katika jela ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala huo.
Faraan: Amina Hamid amesema kuwa utawala haramu wa Israel umeingiza kwa makusudi virusi vya corona katika jela ya mateka wa kike wa Kipalestina ili kuwashinikiza zaidi mateka hao.
Mjumbe huo mwandamizi wa Jihad Islami ameongeza kuwa, hawakushangazwa na habari ya kuambukizwa corona mateka wa kike wa Kipalestina katika jela za Israel hususan kwa kutilia maanani mazingira magumu sana wanayokabiliana nayo ili kuwavunja moyo. Amina Hamid amesema kuwa, Idara ya Magereza ya Israel imetosheka kwa kuwatenga na kuwaweka karantini mateka wa kike wa Kipalestina waliopatwa na virusi vya corona bila ya kuwapa huduma yoyote ya matibabu.
Ameongeza kuwa mateka wa kike wa Palestina wanasumbuliwa na hali mgumu katika jela za Israel na kwamba wamenyimwa ruhusa ya kukutana na familia na mawakili wao.
Ripoti zinasema, jela ya Damun peke yake ina mateka 33 wa kike wa Palestina ambao wamewekwa karantini.
Mwaka uliopita wa 2021 utawala wa Kizayuni wa Israel uliwatia nguvuni mateka 178 wanawake wa Kipalestina ikiwa ni ongezeko la asilimia 32 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.