Jinai mpya ya Marekani Somalia, Biden ameua Wasomali 465

Shirika linalochunguza mashambulizi ya anga ya kimataifa limefichua kuwa Marekani inaficha idadi halisi ya vifo vya raia nchini Somalia na kwamba idadi ya waliopoteza maisha katika nchi hiyo ya Afrika ni mara 30 zaidi ya ile iliyotangazwa na Pentagon.

Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti ya “Truthout”, mashambulizi ya anga ya Marekani nchini Somalia katika miezi ya hivi karibuni hayajaangaziwa sana na vyombo vya habari vya Marekani, na mashambulizi hayo yameua zaidi ya raia 20 katika kipindi cha wiki iliyopita.

Tovuti hiyo imenukulu ripoti ya Shirika linalochunguza mashambulizi ya anga ya kimataifa linalojulikana kama  Airwars la Uingereza, kwamba majeshi ya Marekani yameishambulia kwa mabomu Somalia angalau mara 16 wakati wa urais wa Joe Biden, na kusababisha vifo vya kati ya watu 465 na 545.

Hujuma zote hizo zimefanyika tangu Joe Biden alipoidhinisha kutumwa tena kwa mamia ya wanajeshi wa kikosi maalum cha Marekani nchini Somalia mwezi Mei, na hivyo kubatilisha uamuzi wa rais wa zamani Donald Trump wa kuondoa askari wa Marekani katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Hata hivyo wataalamu wanasema kuwa kujiondoa Trump kutoka Somalia kulikuwa ni “kuhamishia tu wanajeshi katika nchi jirani za Djibouti na Kenya, na kuruhusu mashabulizi yaendelee kupitia ndege zisizo na rubani (drone)”.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo lisilo la kiserikali linalofuatilia mashambulizi ya anga ya kimataifa, tangu mwaka 2007, jeshi la Marekani limefanya mashambulizi 260 nchini Somalia.

Somalia iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi karibuni pia imeshuhudia mashambulizi ya kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Al-Shabaab ni kikundi cha kigaidi chenye silaha ambacho kilianzishwa mapema mwaka wa 2004 na kina mielekeo ya kiitikadi inayoshabihiana na kundi Al-Qaeda.

Magaidi wa Al Shabab wamekuwa wakiua raia katika mji mkuu wa Somalia Mgodishu na maeneo mengine ya nchi hiyo na pia nchi jirani. Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika wako nchini Somalia kukabiliana na kundi hilo la kigaidi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *