Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama yasisitiza kuondolewa haraka vikwazo dhidi ya Syria

Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama imetoa taarifa ikisisitiza udharura wa kuondolewa haraka iwezekanavyo vikwazo dhidi ya Syria katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo inahitajia misaada kutokana na kukumbwa na janga la tetemeko la ardhi.

Taarifa ya Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama imebainisha kwamba, vikwazo vya Marekani dhidi ya Syria ambavyo kimsingi vinakinzana wazi kabisa na hati ya Umoja wa Mataifa na viko kwa maslahi ya adui Mzayuni vimewekewa nchi hiyo ya Kiarabu katika fremu ya siasa zisizo za kiadilifu za Washington.

Taarifa hiyo ya Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama imetolewa baada ya kumalizika mkutano wake katika mji wa Sayda kusini mwa Lebanon uliokuwa ukijadili matukio yanayohusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria na kusisituiza kwamba, kuna ulazima wa kuondolewa haraka vikwazo na mzingiro dhidi ya taifa la Syria.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Marekani imetangaza kwamba imelegeza baadhi ya vikwazo vya Syria kwa siku 180 ili kuwezesha miamala ya kupelekea misaada kwa waathiriwa wa mtetemeko wa ardhi. Marekani imelazimika kufanya hivyo kutokana na mashinikkizo makali ya kikanda na kimataifa kutokana na maafa makubwa ya watu waliokumbwa na mtetemeko wa ardhi nchini Syria.

Hata hivyo walimwerngu wanataka vikwazo hivyo viondolewe vyote hasa katuika kipindi hiki ni si kulegeza baadhi ya vikwazo hivyo.

Katika ziara yake nchini Syria, Tedros Adhanom Ghebreyesus Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) jana alizindua ombi la kibinadamu la kukusanya dola milioni 43 kusaidia juhudi za kukabiliana na athari Syria na Uturuki baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyozikumba nchi hizo mbili wiki moja iliyopita na kusababisha vifo, watu kutawanywa na kujeruhi makumi ya maelfu ya watu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *