Mambo yalivyo nchini Ukraini, huku Urusi ikiwa na shughuli maalum mashariki mwa nchi hiyo

Katika kujibu ombi la usaidizi wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa eneo linalotaka kujitenga la mashariki mwa Ukraine, rais wa Urusi aliamuru operesheni maalum kwenye eneo hilo linaloitwa Donbas.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru Jeshi la Urusi kuanzisha operesheni maalum katika eneo la Donbas; Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema katika taarifa yake kwamba vikosi vya Urusi vinatumia silaha katika operesheni zao maalum ili kufunga miundo mbinu ya kijeshi ya Ukraine na mifumo ya ulinzi wa makombora.

Putin alisema agizo hilo limekuja baada ya viongozi wa eneo lililojitenga la mashariki mwa Ukraine kutoa wito wa usaidizi wa kijeshi wa Urusi katika kukabiliana na kuongezeka kwa “ukiukaji wa sheria nchini Ukraine.”

Baada ya Rais wa Urusi Vladmir Putin kutangaza kuanzisha operesheni maalum ya kijeshi kulinda eneo la Donbas, vyombo vya habari viliripoti sauti ya milipuko katika miji kadhaa ya Ukraine alfajiri ya kuamkia leo.

 

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *