Kamanda Wagner atishia kulipiza kisasi kwa jeshi la Urusi

Yevgeny Prigozhin, ambaye ni kamanda wa kundi la kijeshi la Wagner nchini Urusi, alitangaza kwamba askari wake walikuwa wameanza kuasi amri ya jeshi la Urusi.

Katika ujumbe mwingine, kamanda wa kundi la Wagner alisema kuwa vikosi vyake vimeingia katika mji wa Rostov kusini mwa Urusi kutoka Ukraine na wako tayari kwenda hadi mwisho kukabiliana na jeshi la Urusi.

Prigozhin pia alimshutumu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu kwa kuamuru kulengwa kwa vikosi vya Wagner nchini Ukraine. Alisisitiza kuwa Shoigu hana ujasiri wa kudhibiti Kiev.

Prigozhin aliwaalika Warusi, haswa jeshi la Urusi, kujiunga na safu yake na kutishia jeshi la Urusi kwa kulipiza kisasi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilikanusha taarifa ya Prigozhin na kuyataja madai ya kulipua kambi ya Wagner kuwa ni mvutano wa vyombo vya habari.

Ikulu ya Kremlin pia ilisema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin anafahamu maendeleo yanayohusiana na Wagner na alikuwa amechukua hatua zinazohitajika.

Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi ya Russia pia ilitangaza kuwa Kamanda Wagner atahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa vitendo vyake vya hivi majuzi.

Vyombo vya usalama vya serikali ya Urusi vilizingatia matamshi na tabia ya Prigozhin kama mwaliko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na vikaanza kumchunguza kwa tuhuma za kuchochea uasi wa kutumia silaha.

Moscow ilipitisha usiku wa wasiwasi, hivyo kwamba magari ya kijeshi yalitumwa katika maeneo yake mengi, haswa maeneo ya kijeshi na nyeti.

Inapaswa kusema kuwa mvutano huu pia umehamishiwa Amerika. Baraza la Usalama la Taifa la Marekani lilitangaza kuwa Washington inafuatilia matukio nchini Urusi na itashauriana na washirika wake kuhusu hilo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *